Pages

Jumanne, Machi 18, 2014

SIMULIZI "RAFIKI WA MAWANAMKE"

"Leo lazima nikuvunje miguu yote miwili mchawi mkubwa wewe" Ilikuwa ni sauti yenye hasira kali ikisikika, huku sauti ya mwanamke aliyekuwa anaongea kwa unyonge na kuomba msaada ikisema "Jamani unaniua mume wangu. Mama nakufa nisaidieni jamani nakufa" Jirani kulikuwa na wakinamama wameketi huku wakisemeshana "Yaani huyo mwanamke ni mjinga sana inamaana kupigwa kote huko bado anaendelea kuishi na huyo bwana" Dada mmoja akaongeza neno "Yaani hata mimi namshangaa sana huyu Mwanadodo, kwanza muache apigwe hadi atolewe macho, mimi wala sijali anayataka mwenyewe, kila siku tunaamua ugomvi tunamwambia aondoke huyu mwanaume hamfai, atakuja kumuua lakini mwenzetu hakomi, hata kama ni mapenzi mimi siwezi unaweza kufa hivihivi unajiona".

 Mmoja kati ya wale kidada aliyekuwa anaitwa Subira alisimama nakusema "Lakini jamani pamoja na yote twendeni tukamsaidie mwenzetu" Wote walimcheka na kunyanyuka huku wakiondoka na kumuacha Subira akielekea katika kile chumba alichokuwa akisikia sauti ya Mwanadodo Aligonga mlango bila ya mafanikio, akiwa ameendelea kusimama pale mlango ulifunguliwa na mume wake Mwanadodo alitoka bila ya kuzungumza chochote na kubamiza mlango kisha kuondoka na kumuacha Subira akiwa ameduwaa. SIMULIZI HII INAKUJIA HIVI KARIBUNI USIKOSE KUISOMA HADI MWISHO WAKE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.