Kila kukicha kumekuwa na matukio mbalimbali ya migogoro katika mahusiano ya kimapenzi yakisabishwa na wivu wa kimapezi na kupelekea ugomvi baina ya mke na mume au wapenzi na kufikia hatua ya kuuana. Huko Morogoro mwanamke mmoja Juliana Wambura(24) mkazi wa kijiji cha Ruaha,ameuawa kwa kuchomwa kisu Tumboni na mumewe chanzo ikiwa ni wivu wa kimapenzi.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile amesema Marehemu aliuawa kinyama kwa kuchomwa na kisu tumboni na mumewe aliyefahamika kwa jina la Fredi Ernest (34) mkazi wa Shirati Mara, na kupelekea utumbo wa mkewe kutoka nje. Na baada ya kutekeleza mauaji hayo mtuhumiwa amekimbia. Bado anatafutwa na akipatikana sheria itachukua mkondo wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.