Pages

Jumanne, Machi 04, 2014

USIJE MJINI


Baadhi ya vijana wamekuwa wakihamia toka vijijini kwenda mijini kwa lengo la kupata mafanikio ya kimaisha ikiwemo kuajiriwa au kufanya biashara ya aina yoyote ile bora mkono uende kinywani. Kilimo kimekuwa hakiwavutii baadhi ya vijana, na kujikuta wakizurura au kufanya shughuli ambazo hazina tija.Kutokana na utafiti wadau mbalimbali wanasema vijana wengi wanapenda kuja mjini kutokna na utandawazi pamoja na kushawishiwa na marafiki pamoja na ndugu waishio mijini kuwa wanaweza kupata maisha mazuri.

 Lingine ni kukithiri kwa umasikini vijijini kwenye baadhi  ya familia ambazo  hushindwa hata kumudu angalau milo mitatu kwa siku, lakini wapo vijana ambao wanakimbia kufanya shughuli za kilimo na kutamani kuja mjini kupata ajira au kufanya biashara huku wakiamini kuja mjini unafanikiwa haraka na ndiyo maana unakuta wengine wanajiingiza kwenye biashara ya madawa ya kulevya, ukahaba kuwa wezi na kuzurura ovyo. Serikali inatakiwa kuangali hali halisi ilivyo vijijini na kutafuta ufumbuzi wa haraka vinginevyo vijana wataendelea kukimbilia mijini na kusababisha vijijini kukosa wazalishaji wengi wa mali hasa vijana.USIJE MJINI BILA KAZI NA MALENGO MAALUMU.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.