Ikiwa kila mwaka tarehe nane mwezi wa tatu tunaadhimisha siku ya wanawake. Kuna changamoto nyingi sana wanazopitia wanawake katika maisha ya kila siku ikiwemo tatizo la wanaume kuwatelekeza wanawake, unaambiwa kwa macho ya kawaida ni jambo la kawaida kwa mwanaume kumpa mimba msichana kisha kumtelekeza. Huku akijiona ni shujaa na kidume hasa, lakini kimaadili ni roho mbaya ya kishetani.
"Wasichana wengi wametelekezwa kwasababu wapo masomoni au ni walemavu na wanaume wengine wanawapa mimba hata wenye magonjwa ya akili. Wanajua fika kuwa kitendo hicho kikifanywa bila kinga kuna mawili maradhi au mimba, lakini bado wanaendelea kufanya hivyo wakijua kabisa nni matokeo yake. Na sasa wanapokuja kuona matokeo ya mimba huruka kimanga hata kama wamefanana na watoto hao kama shilingi. Badala ya kuwasimanga wasichana wanaopewa mimba na kutelekezwa, ni vyema nguvu zikawekwa kwa wanaume wanaowapa mimba wasichana hasa ikithibitika mtoto ni wakwake." MANENO YA MCHUNGAJI NEHEMIA YAKOBO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.