Pages

Ijumaa, Machi 07, 2014

SOMA KISA HIKI MAMA AMTETEA BINTI YAKE ALIYESHIKWA UGONI

Mama mmoja anayetoka Wilaya ya Bugongi nchini Uganda amewashangaza majirani na wazee, baada ya kuamua kumtetea binti yake aliyeshikwa ugoni. Mume wa mwanamke huyo alirejea nyumbani jioni na kukuta watoto wake  watatu wakiwa peke yao jikoni. Alipowauliza watoto mkewe Kamirembe yuko wapi, watoto wakamjibu aliondoka wala hawajui alipo.

 Mume akasubiri kwa saa moja,kisha akawatengea watoto chakula cha jioni na kwenda kulala. Baadaye kidogo, mtoto mmoja akaomba apelekwe kujisaidia na ulikuwa umbali wa kama mita 50 hivi. Mume alipofika maliwatoni, jamaa mmoja mwanaume aliruka kutoka huko akifuatiwa na Kamirembe aliyeanza pia kukimbia. Mume naye akaanza kutimua mbio hadi akamkamata mkewe na kumchukua hadi nyumbani.


Asubuhi ya kesho yake alimpeleka kwa wazazi wake na kuwaomba wamshauri kuacha tabia ile chafu. Wazee na wakuu wa ukoo, wakamweka chini Kamirembe na kuanza kumfunda. Hata hivyo wakati wakiendelea Mama mzazi wa Kamirembe alivamia mkutano huo na kusema "kama angekuwa ameshtakiwa kwa wizi, kutokuwaangalia watoto au kumtukana mumewe ningekubali, lakini kumshutumu kwa kufanya Ngono na mwanaume mwingine mimi sikubali kabisa, alichofanya ni sawa, kwani ni kama vile amepiga kura ya kutokuwa na imani na mumewe, alitarajia binti yangu aishije ikiwa hakuwa anapata vyakutosha kile alichokuwa anahitaji?" Kuona hivyo Kamirembe aliondoka mkutanoni, huku akisema mkewe ameharibiwa na Mama yake, hivyo akaondoka na watoto aliokuwa amekwenda nao, huku akiapa kuwa Kamirembe asirejee tena nyumbani kwake. KUTOKA BUGONGI, UGANDA CHANZO HABARI LEO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.