Pages

Ijumaa, Oktoba 15, 2010

Kijana ambaka bibi mwenye umri wa miaka 70..sijui tunaelekea wapi jamani.

    Wakina bibi kama hawa pichani wanakutana na matatizo mengi sana likiwemo la ubakaji na ushirikina.Huko Bagamoyo kuna kijana amembaka bibi wa umri wa miaka 70 na kumjeruhi sana sehemu zake za siri.Tukio hilo lilitokea majira ya usiku wa kuamkia jana wakati bibi kizee huyo ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa amelala alifanyiwa unyama huo na kijana ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Manda A kijijini hapo.akizungumza na Mwananchi Kamanda wa polisi mkoa wa pwani amesema mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kunyata na kufungua mlango wa mbele wa nyumba ya kizee huyo na kuingia moja kwa moja chumbani na kumziba mdomo na kuanza kumbaka.

     Baada ya tukio mtuhumiwa alitokomea kusiko julikana. na bibi huyo alijikokota na kuomba msaada kwa majirani ambao walimpeleka hospitali na kwa sasa anaendelea na matibabu.Kamanda amesema juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea na kuomba wananchi wa kata ya Miono Bagamoyo kutoa ushirikiano wa kumkamata kijana huyo..mmmh sijui tunaelekea wapi wadau inamaana huyu kijana alikuwa anafikiria nini kufanya kitendo cha kinyama kiasi hiki.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.