Pages

Jumapili, Oktoba 17, 2010

Makeup kwa ngozi ya mafuta.


Unaponunua kipodozi cha aina yoyote lazima uangalie na aina ya ngozi uliyonayo kwani vipodozi vyote vimeandikwa aina ya ngozi na ukishajua hilo basi nunua kipodozi kinachoendana na ngozi yako kwa mtu mwenye ngozi yenye mafuta hakikisha unasafisha uso mara kwa mara na "facial clenser" tena zingatia sana kabla ya kulala uhakikishe uso wako umeusafisha vizuri,kama umekosa bidhaa hiyo unaweza kutumia hata maji.wakati unasafisha uso hakikisha unatumia kifaa laini na pia hakikisha hausugui uso kwa nguvu,maana vinginevyo utasababisha ngozi yako kuwa ngumu.

Hizi ni baadhi ya makeup ambazo zinapatikana madukani na inabidi kuwa makini wakati wa kununua kulingana na aina ya ngozi,tumia vipodozi ambavyo havina mafuta kabisa ambavyo ni maalumu kwa ngozi yenye mafuta,pia unaweza kupaka maji ya matango kwenye uso wako kabla ya kupaka makeup inasaidia kwenye muonekano wa ngozi,
Tafuta foundation ina Titanium dioxide ambayo pia inakusaidia kujikinga na jua,,ukitaka kuwa na ngozi yenye mvuto basi hii ndio siri yako kama ngozi yako ina mafuta,jaribu kuwa makini waone wataalamu kwa msaada zaidi kuliko kuiga au kubahatisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.