Pages

Alhamisi, Oktoba 14, 2010

Mmmmh Tattoo ni urembo,,lakini ukizidi mmmmh

Ingawa si watu wengi ambao wanapenda kuchora tattoo mwilini kwasababu mbalimbali lakini tattoo zina mvuto kama zitachorwa katika hali ya kuvutia,ili tattoo zikutoe vizuri ni lazima kufahamu aina ya michoro hiyo na mahitaji yake.bila kujua maana yake basi haina haja ya kuchora mwili wako,kuna sababu nyingi zinaweza kumfanya mtu kuchora tattoo kwanza kutokana na mahitaji ya kijamii (kabila) na pili kama sehemu ya mahitaji ya sanaa ya urembo.
Katika suala la sanaa ya urembo wengine  wanafanya hivyo kama kivutio cha mapenzi,lakini wengine ili kupata umaarufu kwa kuwa tofauti,wengine  huchora sehemu zilizojificha,na wengine huchora sehemu za wazi ili zionekane na kila mtu.

Uchoraji wa tattoo ni sehemu ya urembo kama ilivyo,  kwa wanaovaa shanga,mikufu au kutoga masikio,lakini kama tattoo zitachorwa vibaya zinaweza kuonekana kama uchafu mbele za wengine.

Maoni 3 :

  1. Sijajua kwa nini watu hawaridhiki na uzuri walionao? Kaaazi kwelikweli.

    JibuFuta
  2. Yaani mimi nalaani hadharani kwamba sipendi haya madudu dada yangu, nakama girl wangu atanijia siku kachora huu uchafu, basi ajuwe ndio mwanzo na mwisho wa mahusiano yetu!!

    JibuFuta
  3. @Yasinta umeonaeeeh wengine wanaiga,halafu baada anajuta baada ya umri kwenda@Hashir hahahha tuko pamoja

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.