Pages

Jumatano, Oktoba 06, 2010

Sio vizuri kuficha chakula,,tena mgeni akiwepo ndio mbaya zaidi..tusinyimane chakula jamani..

Kuna baadhi ya watu ni wachoyo hadi kwenye chakula,,yaani anadiriki hata kuficha uvunguni chakula kuliko akigawe au bora akimwage,hizi ni tabia kwa baadhi ya watu mbalimbali.Na uchoyo huu unakuta wanafanyiwa ndugu,jamaa,na marafiki.mwingine unakuta mawifi au ndugu wa mume wake wamekuja nyumbani kusalimia..chakula kipo lakini akakificha asiwakaribishe.na pia inawezekana ikawa ni tabia ya mtu lakini sio tabia nzuri kwani jamani kuna leo na kesho,,leo unacho kesho hauna..sasa huo uchoyo hautakufikisha popote..na hili mara nyingi linawagusa wanawake,,na  pia ni moja kati ya chanzo cha migogoro katika nyumba baina ya wapendanao..mwanaume au mwanamke akiwa mchoyo haipendezi  





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Unakaribishwa kutoa maoni yako.