Pages

Jumapili, Oktoba 03, 2010

Wapo baadhi ya wanaume hulia na kudondosha machozi katika mahusiano,,

Kilio cha mwanamume katika mahusiano,kinaweza kutokana na sababu mbalimbali ,,kusalitiwa,kukataliwa penzi, kudanganywa na baadhi ya wanawake,utakuta mwanamume amemsomesha mwanamke kuanzia Sekondari hadi chuo,lakini mwanamke baada ya kupata kazi anaolewa na mtu tofauti,ni kitendo ambacho kinaumiza sana kwa yule aliyetendewa,ndio maana hata baadhi ya wanaume hujikuta hawana mapenzi ya dhati tena kutokana na kutendwa.

Katika kulia hali hii huwa inatofautiana,kuna yule ambaye atalia kwa uchungu kutokana na mabaya aliyotendewa huku moyoni akiwaza namna ambavyo atalipiza kisasi,na hii huwa mbaya zaidi.kulia katika mahusiano haiangalii mwanamke au mwanamume,ijapokuwa maumivu yanatofautiana..na kuna baadhi ya watu hudiriki kusema wanaume huwa hawaumii sana kama wanawake,,mmmh ,,sijui mnalizungumziaje hili wadau............

Maoni 7 :

  1. Kweli wanaume huwa wanalia Adela,na ukiona mwanaume analia ujue ameumizwa kweli kweli.

    JibuFuta
  2. Wanaume huumia kama wanawake tu ila jamii inamchezo wa kufanya ionekane kitu cha ajabu dume zima likilia.Lakini kulia ni bomba la dawa na karibu mara zote ,ukimaliza kulia utajisikia vizuri. :-(

    JibuFuta
  3. @Edna asante tuko pamoja@Simon hahahha ni kweli bora kulia kuliko kubaki nalo moyoni..

    JibuFuta
  4. Sioni tofauti kulia kwa wanaume na wnawake kwani si wote binadamu au?

    JibuFuta
  5. NDIO DADA YASINTA WOTE TU SAWA ILA WANAUME HAWAUMII KAMA WANAWAKE ME NAVYOONA,

    JibuFuta
  6. Mmmm yaani awe mwanaume au mwanamke anapokuwa na upendo wa dhati kwa mwenzie halafu anaachwa, au anazulumiwa, uchungu ni ule ule kwa wote hivyo kulia hakuna cha mwanaume wala mwanamke.

    JibuFuta
  7. nahitaj ushauri jaman mm ni kijana wa umri wa miaka 22 nafanya kazi kampun moja hv ya madin nilikuwa na mpenz wangu ambae ktk mahusiano yetu bado hatuja fikisha hata mwaka mmjo lakin huyu mtu ameanza kuniletea vituko mara anasema natoka na mwanamke flan yaan anataja jina ambalo mtu mwenyewe simjui alafu amekomaa kwel kuhusu huyo mwanamke na wakat mm sijui chochote kiukweli ananiumiza kichwa sana..NAHITAJI USHAURI WENU IKIWEZEKANA KUPITIA KWENYE [Chakeemanuel@yahoo.com]

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.