Ni vizuri kumkubali mwenzio katika hali yoyote na kuheshimu kile anachokipenda,usimkebehi na mara nyingi walio wengi wanatofautiana vile wanavyovipenda.kuna anayependa kilevi mwenza wake hapendi nk.lakini katika hali kama hii ni vizuri heshima ikachukua mkondo wake na utani usizidi kipimo..kwani wengine huishia kuachana na kugombana kutokana na kukosekana na uwiano baina yao. |
Ni kweli kabisa hayo unayosema ndugu yangu kwani ni vizuri kujaribu kuwa uwiano hata kidogo vinginevyo utakuwa unaumia tu
JibuFutaInawezekana kumpata mtu ambaye mna uwiano lakini isiwe ni katika kila kitu ila kama ulivyosema Adela ni vizuri kuheshimu kile anachokipenda mwenzio na si kuweka dharau
JibuFutaUpendo wa dhati hutoka moyoni. Nakumbuka siku moja babu yangu aliniambia kuwa utagundua tu huyu ni mke na mume wakiwa barabarani au akiongea na simu.
JibuFuta'Watu wanakua kama wapo katika ugomvi, kuongea kwao kama vile hawataki, na kwenye simu utasikia `ehe, sema, kwani vipi..., lakini awe anaongea na mpenzi wake au nyumba ndogo...mmmh, vipi shosti, vipi mpenze, nimekumiss...'
Kwaweli niliamua kufanya uchunguzi na ukiangalais asilimia kubwa ndivyo ilivyo. Watu wamekaa ndani ya gari kama wanatoka kugombana, akipigiwa simu anakunja uso...jamani hamumuogopi mungu, au hamuitaki pepo...
Sijui, nawaza tu ndugu yangu Adela