Pages

Jumatano, Oktoba 10, 2012

"Ni vyema wanaowatelekeza watoto wa nje ya ndoa wawajibishwe

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume au wanawake kuwatelekeza watoto waliozaliwa nje ya ndoa  na hivyo kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani , Ni vyema katiba ijayo ikaweka wazi jambo hilo ili kuwadhibiti wanaume wasizae ovyo na pia kuondoa watoto wa mitaani  hayo yamesemwa na mkazi wa Rau Balbina alipokuwa akitoa maoni yake mbele ya Tume ya mabadiliko ya katiba mpya 

hivyo ili kudhibiti watoto wanaozaliwa nje ya ndoa vipimo vya DNA vitumike kubaini baba halali na wawajibishwe kuwatunza kwani watoto wengi wa mitaani wametokana na wazazi kutengana au kukataliwa na wazazi wao hususani wanaume  hivyo Katiba ikiwa na mwongozo kuhusu jambo hilo ni wazi kwamba tatizo  la watoto hao litakwisha

Maoni 1 :

  1. Hawa wanaofanya hivyo, wanajitakia laana, kwani mlipokuwa mnalima mlitajia nini,...ni kuvuna na hayo ndiyo mavuno,kwanini mnayacha yaozee yashambani?

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.