Pages

Jumatano, Novemba 07, 2012

MWANAMUZIKI RAY C ANAHITAJI MSAADA WAKO MDAU

Kutokana na kuwa na matatizo ya kuathirika na madawa ya kulevya  Ray c msanii wa bongo fleva anahitaji msaada wako ili kupata matibabu ya  kuondokana na tatizo hilo

kwa mujibu wa maelezo ya mama yake mzazi Ray c    dawa anazotakiwa kutumia ni gharama lakini pia gharama ya chakula kwa mgonjwa, wapenzi wamuziki na wadau mbalimbali wa mwanamuziki huyu  tunaweza kumsaidia mama huyu  kwa kumtumia kiasi chochote cha fedha kwa kutumia huduma ya tigo pesa 0655999700 

Habari hii kwa hisani Mwanamuziki Mkongwe MZEE Kitime lakini pia unaweza kuingia michuzijr.blogspot.com 

kiuno bila mfupa RAY C ukweli ni kwamba amekiri makosa ya kutumia madawa  ya kulevya na hivyo kwa sasa anahitaji msaada KUTOA NI MOYO 



Maoni 2 :

  1. Jamani jamani mnayaona haya, kuna wadau niliwaambia haya hayana ushabiki, hili ni janga, madawa ya kulevya, ushoga, nk,haya yanatokea huko nje, haijalishi ni wapi, hatuwezi kubishana kiushabiki kuwa yanatoka mashariki au ulaya au Marekani. Kinachotakiwa ni nguvu za pamoja za kupambana na hili janga.

    LEO ni kwa huyu mwanadada,ambaye wengi wanamfahamu kwa kazi yake ya muziki, kesho atakuwa mwingine, na kuna wengi hawajulikani kwasababu hawana majina, wanataabika kwelikweli.
    Mimi naona ni vyema, serikali ikaliangalia hili kwa undani zaidi. Mimi naona kuwe na chuo, maalumu cha kuwahifadhi hawa watu, humo kuwe na huduma mbali mbali ikiwemo ushauri nasaha, maana sio kwa huyu mwanamziki tu, wapo wengi mitaani.
    Kutoa ni moyo na wala sio utajiri.

    JibuFuta
  2. Jamani nampa pole sana mama yake Ray C, maana ray c alifanya kwa stgarehe zake lakini sasahiv anasumbuka ni mama yake. jamani watanzania tujifunze sana kwa hili janga tusiige wenzetu, leo ni ray c kesho ni wewe. Usupastaa sio kuiga hata mambo ambayo hayafai kuwa na uhalisia wako.
    Tumsaidie jamani ni mtoto wetu.

    mama B wa Kimara Baruti

    JibuFuta

Unakaribishwa kutoa maoni yako.