MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA....“Mume wangu hii bahasha ndani ina ujumbe kuna msichana ameiletanimpe Jamal nimefungua nikasoma niliyokutana nayo nimeshindwa kuamini macho na akili yangu nimeona nikupe kwanza uisome uone mambo anayofanya mtoto wako.” JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA 12
INAPOENDELEA
Jamal
alichukua ile barua na kutoa karatasi yenye ujumbe
uliosomeka
hivi:
“Kwako
mpenzi Jamal ni matumaini yangu umzima wa afya, vipi
unaendeleaje
na maisha? Kwa nini umenitupa hivyo? Je, unajua ni
kwa kiasi
gani niliteseka nilipotoa ile mimba yako? Sawa bwana! Ila
mimi bado
nakupenda mpenzi wangu. Vipi shule utakwenda lini?
Naomba
tuonane kabla hujaondoka ili nikupe ile zawadi uipendayo.
Ni mimi
mpenzi wako Maria.”
Alipomaliza
kusoma ule ujumbe baba Jamal alikunja uso na kuitupa ile
barua
chini huku akisimama na kufoka kwa hasira.
“Hivi huyu
mtoto amekuwa mwendawazimu kiasi hiki! Yaani mimi
nahangaika
kutafuta fedha ili nimpeleke shule akasome yeye anawaza
mapenzi!”
Alifoka baba Jamal.
“Ndiyo hali
halisi mume wangu, Jamal hawezi kusoma kabisa. Kwa hiyo
utajijua
mwenyewe kusuka au kunyoa. Nionavyo mimi hapa utapoteza
fedha zako
bure. Kama ameshindwa kufanya vizuri Kidato cha Nne ndo
atamudu
Kidato cha Tano?” Alitamka na kuuliza mama mdogo kwa
dharau. “Nashukuru
sana kwa taarifa, nadhani sasa siwezi kupoteza fedha zangu kwa huyu
mjinga. Kwanza yuko wapi sahizi?” Aliongea baba Jamal na
kuuliza. “Nadhani
atakuwa huko chumbani kwake akiangalia mikanda ya video, si ndio kazi
yake.” Alijibu mama mdogo. “Jamal!
Jamal!” Aliita baba Jamal kwa sauti.
“Naam
baba!” Aliitikia Jamal huku akisimama na kuelekea sebuleni.
Alipofika
tu kabla hata hajaongea chochote baba yake alimpiga Jamal
kibao cha
usoni. Jamal alipepesuka hadi kwenye sofa huku akishangaa na
kutoelewa
kinachoendela. Jamal alishindwa kuelewa sababu ya kupigwa.“
“Baba
mbona unanipiga bila sababu? Kosa langu ni nini?.” Aliuliza Jamal
huku
akibubujika machozi. Baba yake
alichukua ule ujumbe na kumtupia Jamal huku akifoka kwa hasira.
“Unataka
kujua umefanya nini? Leo lazima nikumalize mjinga mkubwa
wewe! Mimi
nakupeleka shule kusoma unakwenda kujifunza mapenzi!
Sasa
nataka uniambie kwa nini umefanya hivi?” Aliendelea kufoka baba
Jamal kwa
hasira.
Jamal
aliokota ile karatasi na kusoma ule ujumbe. Alibaki akishangaa sana
kuona
ujumbe ambao hakujua aliyeandika, na ulimlenga nani.
“Baba
mbona mimi sielewi huyu Mary ni nani, mimi simjui baba sidhani
kama huu
ujumbe utakuwa ni wa kwangu.” Aliongea Jamal kwa kujiamini.
“Nitakuua
Jamal unataka kusema mimi mjinga, sasa sikiliza hutakwenda
shule
utakaa hapa nyumbani hadi akili yako itakapokaa sawa, na tena hii
hali
ikiendelea nitakufukuza hapa nyumbani.” Alifoka baba Jamal huku
amemshika
Jamal shingoni kana kwamba anataka kumnyonga.
“Lakini
baba unanionea mimi sijafanya hivyo na pia napenda kusoma
baba hata
mama aliniambia nisome kwa bidii ili niweze kusimamia mali
alizoacha.”
Aliongea kwa huruma Jamal.
“Hivi wewe
ujasiri wa kujibizana na mimi umeupata wapi? Kosa umetenda
kidhibiti
hiki hapa unakataa nini?Sasa nenda kamfuate mama yako
kaburini
umwambie akusomeshe mpumbavu mkubwa unabishana na
mimi.”
Aliongea baba Jamal huku hasira zikimpanda.
Baba Jamal
aliendelea kumpinga Jamal hadi nguvu zilipomwishia. Mama
yake mdogo
alitabasamu na kucheka muda wote wakati Jamal anapigwa.
Jamali
alifanikiwa kupata kaupenyo na kukimbilia nje hadi mtaa wa tatu.
Jamal
alitembea asijue wapi anaelekea hadi alipofika katika gogo moja kavu
akaamua
kukaa akiendelea kulia kwa uchungu na mawazo mengi sana.
“Laiti
mama angekuwepo! Hivi kwa nini mama umetuacha? Angalia
mwanao
ninateseka bila sababu.” Aliwaza kwa uchungu Jamal.
Baada ya
saa mbili kupita Jamal aliamua kurudi nyumbani. Alipofika baba
yake
hakuwepo sebuleni. Alikaa kimya hadi mama yake mdogo
alipomletea
chakula akala na kwenda kulala. Usiku ule ulikuwa ni usiku
wa majonzi
sana kwa Jamal.
Siku za
kwenda shule Jamal ziliwadia, lakini baba yake hakuhangaika
kumtafutia
shule. Wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano walianza
kwenda
katika shule mbalimbali. Jamal alijaribu kumwomba baba yake
ampeleke
shule, lakini baba yake hakutaka kusikia kabisa. Hivyo aliendelea
kukaa
nyumbani bila shughuli yoyote akitafakari hatima ya maisha yake
na mdogo
wake Aisha endapo hatakwenda kusoma.
“Wenzangu
wameshakwenda shule mimi bado nipo nyumbani na yote
haya ni
kwa sababu ya mama mdogo. Baba naye amebadilika sana hataki
kunisikiliza
kabisa, sijui nifanyeje. Natamani sana niendelee na shule.”
Aliwaza
Jamal.
Wakati
akiendelea kuwaza ghafla aliingia rafiki yake Goodluck.
“Jamal
habari za asubuhi” Alisalimia Goodluck.
“Habari
siyo nzuri ila afya yangu safi.” Alijibu Jamal.
“Kwanini
siyo nzuri?” Aliuliza Goodluck.
“Si unajua
matokeo yangu ya mtihani siyo mazuri sana, hivyo
sikuchaguliwa
kuendelea na Kidago cha Tano.” Alieleza Jamal.
“Lakini
kwa daraja la tatu ulilopata unaweza kwenda shule binafsi.”
Alishauri
Goodluck.”
“Ndiyo
lakini baba amekataa katakata kunisomesha, sababu ni huyo mama
mdogo
anamshauri vibaya. Na chanzo ananitaka kimapenzi mimi
ninakataa.
Hivyo alishasema eti kwa sababu ninajifanya mjanja hata hiyo
shule
sitasoma. Huwezi amini ananizushia mambo ya ajabu kiasi kwamba
baba naye
anaamini na sasa ameghaili kunisomesha.” Aliongea Jamal kwa
huzuni na
hisia kubwa.
“Pole sana
rafiki yangu lakini mbona hiyo ni kazi ndogo sana. Ningekuwa
ni mimi
ningemkubalia ilimradi tu amshauri baba anipeleke shule.
Kumbuka
muda ni huu wa kusoma ukichelewa basi hata huyo mdogo
wako
utamsaidiaje?” Alishauri Goodluck.
“Kwa nini
hukunishauri hivi muda wote huu?” Aliuliza Jamal.
“Hukuniambia
Jamal, ningejuaje kama unatatizo?” Aliuliza Goodluck.
“Nakushukuru
sana Goodluck, nadhani sasa itanibidi nikubaliane na ombi
la mama
mdogo kwani ndiyo kikwazo. Halafu nikishakwenda shule
baadaye
nitajua cha kufanya. Jamal uamuzi huu ni mgumu sana, lakini sina
namna
inaniuma sana, Mungu anisaidie.” Jamal alitamka.
Baada ya
maongezi hayo Goodluck aliaga na kuondoka kuelekea kwao
akimwacha
Jamal akiwa na mawazo mengi kuhusu mama yake mdogo.
Siku
iliyofuata yapata saa nne asubuhi wakati babake akiwa kazini Jamal
alimfuata
mama yake mdogo sebuleni ili azungumze naye kuhusu swala
la kupekekwa
shule. Alipoingia tu alimkuta amekaa katika sofa akifuma
kitambaa. USIKOSE SURA YA 13 muendelezo utaendelea hadi mwisho
Nimefurahi sana leo kuiona tena hadithi hii! Mana nilimtuma mtu aninunulie pale salamander alikuta vimekwisha! Usichoke kuiweka kwani inavutia na haichoshi kuisoma! Mpaka hapa nakupa mia kwa mia 100%. Nakutakia afya njema ili utuwekee kila siku hadithi hii.
JibuFutaPAMOJA SANA MUENDELEZO UTAENDELA HADI MWISHO
JibuFutaAsante sana kwa kunijibu! Naisubiri namba 13 ili nione kilitokea nini! Ukipata muda niwekee mshabiki wako namba 1 nifurahi na moyo wangu.
JibuFuta