Wakati hapa nchini wanawake wanaonyonyesha hufanya hivyo sokoni barabarani na hata kwenye mabasi ya abiria nchi nyingi zinazoendelea zinapiga marufuku wanawake kunyonyesha hadharani. Wanawake wengi katika nchi za Marekani, Uingereza, Ubelgiji na ujerumani wamekuwa wakikatazwa kunyonyesha hadharani na kitendo hicho kilionekana kama uchafu, kujianika au kufanya kitendo kama mtu asiye na nyumba.
Hospitali nyingi katika nchi hizo zimebandika matangazo yanayokataza wanawake kunyonyesha wakidai kuwa kunyonyesha hadharani kunawadhalilisha wanawake. Mwanamke mmoja anaitwa Emily alibandikwa bango lililoandikwa "asiye na makazi" Baada ya kunyonyesha hadharani.Baada ya tukio hilo Emily aliwakusanya wanawake wengine 1000 wanaonyonyesha na kuanza kuzunguka katika vitongoji vya Uingereza huku wakinyonyesha watoto wao hadharani.CHANZO MWANANCHI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Unakaribishwa kutoa maoni yako.