MTUNZI: ADELA DALLY KKAVISHE
KITABU MALIPO NI HAPAHAPA KIPO MTAANI KWA SASA
EMAIL kavisheadela@yahoo.com
+2550652343430
ILIPOISHIA....“Usijali kuhusu hilo mpenzi, kwani mimi nilichoamua hakuna anayeweza
kunipinga. Wewe ndiye utakuwa mama mwenye nyumba kuanzia sasa. Hapa ni kwako
sawa mamaaa?” Alisema Mzee said kwa kujiamini huku akicheka.
INAPOENDELEA...Mzee Said aliamua kumtembeza Sophia pale nyumbani na kumwonyesha
mazingira yote. Tangia siku ile Sophia aliishi na Mzee Said kama mke na mume na
aliponogewa na mapenzi ya mke mpya aliamua kufunga ndoa harakaharaka bomani
tena kisiri bila watu wengine kujua.
********
Siku moja Jamal aliomba ruhusa kwa mwalimu ili aende Hospitali kutokana
na kusumbuliwa na homa. Baada ya
kuruhusiwa aliamua kwenda nyumbani ili akamtaarifu baba yake juu ya kuumwa
kwake na kisha ampeleke hospitali. Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, Jamal alijua
lazima atamkuta baba yake nyumbani. Alipofika na kuingia getini, aliona gari la
baba yake likiwa limepaki. Jamal alifurahi sana kwani alikuwa na uhakika kuwa
baba yake yupo.
“Afadhali nimemkuta baba.” Aliwaza Jamal na kugonga mlango.
Baada ya kugonga mara kadhaa na kukosa majibu aliamua kuingia ndani na
kuanza kuita.
“Baba! Baba!” Aliita Jamal lakini hakupata jibu.
Wakati huo baba yake alikuwa chumbani amepumzika na Sophia. Baadaye Mzee
Said alisikia sauti ya Jamal ikiita kutoka sebuleni, alitoka haraka kuelekea sebuleni
na kumkuta Jamal.









