Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UJUMBE WA LEO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UJUMBE WA LEO. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, Februari 06, 2014

Jumatatu, Desemba 30, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO "HOFU NA KUKATA TAMAA KUNARUDISHA MAENDELEO NYUMA, KUJIAMINI NA KUTHUBUTU KUNALETA MAENDELEO

Wakati mwingine mtu unaweza kuwa na mawazo mazuri ya kufanya jambo la maendeleo, lakini ukaingiwa na hofu kutokana na mazingira au watu wanaokuzunguka, lakini siku zote, kujiamini na kufanya kile ambacho unakifikiria alimradi  liwe ni jambo halali,  basi lazima utafanikiwa, muhimu kujikubali kwani ukiruhusu hofu lazima utaanguka na utashindwa kusonga mbele.

KILA MTU ANAWEZA KUFANIKIWA JAMBO LA MSINGI NIKUJUA NINI UNATAKA KUFANYA, NA WAPI UANZIE ILI UFIKE PALE UNAPOTAKA, BILA KUKATA TAMAA. kwani siku zote ili ufanikiwe lazima utakutana na changamoto nyingi sana. yote kwa yote jambo la muhimu ni kusonga mbele na utafika tu.

Jumatano, Novemba 13, 2013

UJUMBE WA LEO SAMEHE MARA SABA SABINI, BILA KUWA NA KINYONGO

Katika maisha tunakutana na watu mbalimbali  na wenye tabia tofauti tofauti, na ukweli ni kwamba  maisha tunayoishi kibinadamu huwa kuna makosa tunayoyafanya. Inawezekana ukamkosea yule umpendaye, awe ni mzazi wako, ndugu yako au rafiki yako. Na wakati mwingine mkagombana sana kwa kiasi ambacho inaweza kupelekea kuchukiana maisha yenu yote. 

Kwani kila mtu ana tabia yake kuna mwingine ukimkosea hata ukimuomba msamaha atakuambia nimekusamehe lakini moyoni mwake akabaki kuwa na kinyongo basi ujue mtu huyo hajakusamehe. Unaambiwa samehe mara saba sabini hakuna binadamu aliyekamilika. Lakini pia ni vyema kukiri kosa kwa yule uliyemtendea kosa. TUISHI KWA UPENDO NA AMANI. 

Jumapili, Oktoba 13, 2013

UJUMBE MZURI JUMAPILI YA LEO "MAISHA NI KAMA KITABU"

Maisha ni kama kitabu.Katika maisha kuna walio nafuraha, wapo  walio na matatizo ikiwa ni pamoja na kuishi katika mzingira magumu, magonjwa nk. na yote haya hutokea katika maisha yetu, lakini unaambiwa hakuna kukata tamaa endelea kusonga mbele kwani leo unaweza kuwa na huzuni au maisha magumu lakini kesho maisha yakabadilika na ukawa mwenye furaha jambo la msingi usikate tamaa.

Jumanne, Septemba 24, 2013

UJUMBE WA LEO "SIYO KILAJAMBO UNAWEZA KUVUMILIA"

Katika maisha ni vyema kuwa mvumilivu lakini siyo kila jambo unaweza kuvumilia wakati mwingine unaamua kuacha na kuanzisha safari nyingine katika jambo fulani. LAKINI KUMBUKA MVUMILIVU HULA MBIVU. ILA  UVUMILIVU UKIZIDI SANA UNAWEZA KUJIKUTA UNAUMIA MWENYEWE.

Jumapili, Septemba 22, 2013

NENO LA LEO "UNAPOAMUA KUPAMBANA KATIKA JAMBO LA MAENDELEO BASI USIZIOGOPE CHANGAMOTO, KUMBUKA PENYE NIA PANA NJIA"

Ili ufanikiwe ni lazima utakutana na changamoto nyingi sana, na ili ufikie malengo lazima ukabiliane na changamoto hizo. Pia kumbuka siyo kila anayekuzungukua atafurahia kile unachokifanya  na pia siyo kila atakayekusifia anafurahia unachokifanya. Jambo la msingi ni kujitambua, kujikubali, kujiamini alimradi unao uhakika na kile unachokifanya. ANAYETAFUTA SIKU ZOTE HAOGOPI BALI ANAANGALIA FURSA NA KUSONGA MBELE.

Jumatatu, Septemba 16, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO SIYO KILA JAMBO UNAWEZA KUJITETEA WAKATI MWINGINE INAKUBIDI KUNYAMAZA KIMYA.

Maisha yana changamoto nyingi sana inawezekana unakutana na vikwazo vya hapa na pale lakini bado unasonga mbele,wahenga wanasema ni bora kukaa kimya kuliko kujibizana kwani kwa kufanya hivyo unaweza kuonekana na wewe pia ni mjinga.  WADAU TUENDELEE KUWA PAMOJA NILIKUWA KWENYE MATATIZO KIDOGO LAKINI NAMSHUKURU MUNGU SASA MAMBO YATAENDELEA VIZURI KAMA KAWAIDA 

Ijumaa, Agosti 30, 2013

UJUMBE WA LEO "SIYO KILA JAMBO BAYA UNALOFANYIWA NI LA KULIFUMBIA MACHO NA KUKAA KIMYA, WAKATI MWINGINE HAINA BUDI UTETEE HAKI YAKO

Kuna wakati unaweza kuwa mvumilivu sana katika mambo mbalimbali unayofanyiwa iwe ni katika kazi yako, na marafiki,au katika mapenzi nk. Lakini kuna mambo mengine unaona kabisa hapa sijatendewa haki na wewe ukanyamaza kimya basi ujue unajinyima haki yako ya msingi. Si kwamba ufanye ugomvi ama vita bali kuwa makini nachukua njia sahihi kujitetea ikiwemo sheria.

Jumamosi, Agosti 24, 2013

UJUMBE WA LEO, UKIWAOGOPA WALE WANAOKUCHUKIA KATIKA KAZI YAKO BASI NI VIGUMU KWAKO KUFIKIA MALENGO YAKO"

 Katika maisha ni vyema kuwa makini sana na wasiopenda maendeleo yako kwani wakati mwingine mtu anakuchukia tu bila sababu, hivyo ukikata tamaa na kurudi nyumba anafurahi sana, lakini ukiwa na msimamo na kusonga mbele basi atabaki akikuwaza tu wakati huo mambo yako yanaendelea kuwa mazuri


Jumanne, Julai 30, 2013

UJUMBE WA LEO "UGUMU WA MAISHA, KIPIMO CHA AKILI"

Kupambana katika maisha ndiyo mpango mzima. Ijapokuwa inaweza kufikia kipindi mtu ukakata tamaa kutokana na ugumu wa maisha. LAKINI USICHOKE ENDELEA KUPAMBANA HADI KIELEWEKE, UGUMU WA MAISHA NI KIPIMO CHA AKILI. JARIBU KUTHUBUTU ILI UWEZE KUFIKIA MALENGO YAKO.

Jumapili, Juni 30, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO...DHARAU NI MBAYA SANA ....USIMDHARAU MTU KWA MACHACHE UYAJUAYO KUHUSU YEYE.

Katika maisha ni wazi kabisa kuna baadhi ya watu wanayotabia ya kuwadharau wawaonao, kwa kuwa tu muonekano wao na kazi zao huwatambulisha kuwa watu wa kundi la chini. Usisahau kuwa kila mtu anaweza kuwa msaada katika maisha. Binadamu tunategemeana katika kila jambo. mfano "Bosi unamdaharau na kumnyanyasa msichana wa kazi, basi asingekuwepo huyo msichana wa kazi naimani kazi zote za ndani ungezifanya mwenyewe".

Jumanne, Juni 04, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO, KUWA NA AMANI NA FURAHA MOYONI NI JAMBO LA KUMSHUKURU SANA MUNGU.

UNAPOJISIKIA AMANI MOYONI NA FURAHA SIYO KWAMBA UNAISHI MAISHA MAZURI SANA AU UNA PESA NYINGI SANA BALI NI FURAHA NA AMANI YA KWAMBA WEWE NI MZIMA NA UNAWEZA KUTAFUTA WAKATI WOWOTE, KWANI HATA KAMA UMEKOSA LEO YAWEZEKANA KESHO UKAPATA. PIGA MOYO KONDE KILA KITU KITAENDA SAWA

Jumanne, Mei 07, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO " NI RAHISI KUMUAMINI MTU NA KUWA MARAFIKI KWA KUMUANGALIA LAKINI NI VIGUMU KUFAHAMU NINI ANAKIWAZA JUU YAKO.

Kama ingelikuwa ukimwangalia mtu unafahamu kile anachokiwaza moyoni mwake juu yako. basi ingekuwa rahisi kumtambua rafiki wa kweli. Kwani ungechukua tahadhari mapema ,,,lakini haiwezekani hata siku moja kufahamu nini mwenzio anafikiria juu yako kwani anaweza kucheka na wewe lakini moyoni anakuchukia sana. NI VYEMA KUWA MAKINI SIYO KILA ANAYEKUTAMKIA ANAKUPENDA ANAMAANISHA.

Jumapili, Mei 05, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO NI "UNAWEZA KUWA UNAMPENDA SANA LAKINI UKAWA HAUNA IMANI NAYE"

Katika maisha yawezekana ukawa unampenda sana iwe ni rafiki, mume, mke ama mpenzi unampenda sana na siku zote ukawa ,akiwa katika safari zake kwenye mihangaiko na huku ukimuamini kwamba hawezi kukusaliti kwa namna moja au nyingine na wala usionyeshe wivu juu yake lakini moyoni mwako hauna imani naye. Ni hali ambayo ipo katika maisha yetu kwani binadamu siku hizi wamekuwa vigeugeu, ni vigumu kumuamini mtu kwa asilimia mia moja hata kama ni ndugu yako.

Alhamisi, Machi 21, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO "SIYO KILA MTU MWENYE MANENO MAZURI, ANAYEFUNDISHA NA KUELIMISHA JAMII ANAYATENDA YALE ANAYOYAFUNDISHA.

Inawezekana akawa ni mwalimu mzuri sana wa kufundisha maadili mema katika mambo MBALIMBALI, lakini tabia aliyonayo isiwe nzuri. kwasababu, yale anayoyatenda katika jamii hayaendani  kabisa na vile anavyoelimisha jamii, mfano anawaasa watu wasifanye uzinzi au kutumia kilevi lakini yeye ndiye wa kwanza kutenda mambo hayo  wataalamu wanakuambia "chukua maneno yangu uelimike lakini usiige tabia yangu" TUKO PAMOJA SANA WADAU.


Jumapili, Machi 17, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO "SIYO KILA ANAYEKUSIFIA NA KUKUTAMKIA ANAKUPENDA ANAMAANISHA KUTOKA MOYONI NI VYEMA KUWA MAKINI"

Yawezekana umekuwa na marafiki wengi wanaokuzunguka na kila mmoja ana tabia zake, kuna baadhi ya watu anaweza kuwa karibu na wewe huku akijifanya anafurahia maendeleo yako ama akikusifia katika kila jambo unalolifanya, huku akionyesha kukubaliana na wewe kwa kila jambo, ni wazi kuwa mtu huyu utamuamini na kumuona rafiki mzuri. Lakini wanasaikolojia wanasema "Rafiki wa kweli ni yule ambaye hakubaliani na wewe kwa kila jambo mambo mengine lazima atayapinga" Hata kwenye mapenzi  pia utakuta mtu anakusifia, anakuambia maneno matamu unajisikia furaha kumbe mwenzio kuna kitu anakitaka akishakipata wala hakuna mapenzi. NI VYEMA KUWA MAKINI

Ijumaa, Machi 08, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO SIYO KILA KIN'GARICHO NI DHAHABU NI MUHIMU KUWA MAKINI"

Tunaishi katika mazingira ambayo tunakutana na watu tofauti na wenye tabia za aina mbalimbali, ni vyema kuwa makini na wale waliokuzunguka kwani yawezekana ukawaona ni wazuri sana kwasababu wapo karibu na wewe lakini kumbe sivyo unavyofikiria kwani yawezekana akawa na sura ya upole lakini si mpole, na anaweza kuwa anacheka lakini katika moyo wake hamaanishi hivyo, pia unaambiwa usimtazame mtu kwa mara moja tu kwani uzuri waweza kuwa wa nje tu lakini ndani balaa. MUHIMU KUWA MAKINI.

Ijumaa, Januari 11, 2013

UJUMBE WANGU WA LEO TABASAMU HUONGEZA MVUTO NA MATUMAINI

Binafsi huwa napenda kufurahi wakati wote,, ila mtu akinikwaza najikuta sina furaha ila nitatafuta namna ya kuiondoa hiyo hali ili isiwe kero kwa wengine,Ni kweli waswahili wanakuambia "cheka huongeze siku za kuishi" kununa nuna hakuna maana,, lakini kutokana na mzingira na maisha tunayoishi hali ya kukasirika ni kitu cha kawaida kwani leo unaweza kufurahi kesho ikawa tofauti lakini ni vyema kutafuta njia ya kufurahi na kujipa matumaini kwa magumu unayopitia KUWA MWENYE FURAHA TAFUTA TABASAMU

Ijumaa, Novemba 23, 2012

UJUMBE WANGU WA LEO "SIYO KILA KITU NI CHA KUIGA VINGINE UNAVIACHA KAMA VILIVYO" NAWATAKIA WEEKEND NJEMA WADAU

Kuna baadhi ya mambo ambayo yanafanyika katika jamii iwe ni katika maendeleo, mapenzi nakadhalika ni vyema kuangalia mambo mazuri  na kuiga,  lakini halahala si kila jambo ni la kuiga vingine havifai UMAKINI NI MUHIMU KATIKA KILA JAMBO.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom