Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NYOTA WA LEO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NYOTA WA LEO. Onyesha machapisho yote

Jumatano, Oktoba 23, 2013

MIAKA 10 YA NDOA VAN VICKER

Mchezaji filamu wa Ghana Van Vicker ametimiza miaka 10 ya ndoa na mkewe Adjoa. Wawili hawa walifunga ndoa oktoba 16, 2013. 

Van Vicker na mke na watoto wao.Vicker pia ni mtangazaji wa Radio.


enzi hizo akiwa na mke wake kabla ya kufunga ndoa

ujumbe wake ni kwamba "Penzi nililonalo kwa mke wangu Adjoa halitokufa na badala yake linazidi kuwa imara kila siku" 

Jumatano, Mei 15, 2013

USHAURI WA ANGELINA JOLIE, KWA WANAWAKE BAADA YA KUKATWA MATITI KUZUIA SARATANI.

Mchezaji filamu mashuhuri kutoka Marekani. Anjeline Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.Ni kutokana na kufanyiwa  uchunguzi wa chembechembe  zake na kugunduliwa kwamba alikuwa na hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti.Anjelina mwenye umri wa miaka 37 na mama wa watoto sita alimpoteza mama yake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti. Kulingana na Jolie madaktari walisema  uwezekano wake kupata saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 za uwezo wa kuugua  saratani ya mfuko wa uzazi

Amesema "Niliamua kuchukua hatua mwenyewe  ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua saratani hiyo alisema Jolie".Kwa mujibu wa BBC , Jolie alisema  kuwa shughuli hiyo ilianza februari na kukamilika april mwishoni.Bi Jolie alieleza kuwa Mama yake alipambana na ugonjwa wa saratani kwa miaka 10 na kufariki akiwa na umri wa miaka 56.Amesema alielewa fika siku moja atawahi kuugua saratani na ndiyo maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti .
Alimsifu mumewe Brad Pitt kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila hatua aliyopitia na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanaye hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji.

Amesema "Ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi nilioufanya nakwakua ninabakia kuwa manamke hata baada ya kuondoa viungo hivyo" na kwa mwanamke yeyote  anyesoma maneno haya natumaini kuwa  anaweza kujua anaweza kuchukua maamuzi kama yangu iwapo atajigundua anazo dalili za ugonjwa wa saratani.Mwigizaji huyu  ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.

Jumanne, Machi 26, 2013

NYOTA WA LEO CHINUA ACHEBE, AMEACHA PENGO KUBWA KATIKA FASIHI. TUTAMKUMBUKA MILELE KWA UWEZO WAKE WA KUANDIKA VITU VINAVYOGUSA JAMII

Aliandika kitabu chake ‘Things Fall Apart’ katika miaka ya 20 kikielezea jinsi wazee wa kikabila wa Nigeria walivyosalimu amri mbele ya  wakoloni wa Uingereza.Kitabu hicho kimetafsriwa katika  lugha zaidi ya 50 na kuuza nakala milioni 8 kote duniani.
Achebe alipooza kutokana na ajali ya barabarani  mwaka wa 1990 na ameishi Marekani kwa miaka mingi tangu wakati huo, akiendelea kutetea demokrasia katika nchi yake asili ya Nigeria.

Baada ya Achebe kuingia chuo kikuu, alipenda zaidi kusoma kazi za wanafasihi wengine, lakini pia alipendelea kuandika hadithi mbalimbali na alipomaliza masomo chuo kikuu aliajiriwa katika kituo cha utangazaji Nigeria NBS.

Alijaribu kuingia katika vyama vya siasa mwaka 1970 lakini aliacha baada ya kushuhudia rushwa na uvunjaji wa sheria uliokithiri.September 1961 Achebe alifunga ndoa na Christine Okeli mfanyakazi mwenzake katika television ya NBS. Walibahatika kupata watoto wanne na ndoa yao inatajwa kuwa yenye amani na upendo thabiti.
Chinua Achebe’s family, his wife Christie (in red), his youngest daughter Nwando and sons Ikechukwu and Chidi (in black).
 

Alhamisi, Novemba 08, 2012

NYOTA WA LEO YVONNE CHAKA CHAKA

Chaka Chaka alizaliwa Dobsonville huko Soweto. Akiwa ni mtoto wa kwanza wa kiafrika kuonekana kwenye televisheni Afrika Kusini. Mwaka 1981 "Sugar Shack" Chaka Chaka alianza kuimba akiwa na miaka 19 mwaka 1985 wakati Phil Hollis wa Dephon Records alimgundua mjini Johannesburg.Muda mfupi baada ya albamu yake "I'm in Love With a DJ", kuuzwa nakala 35,000, wimbo huo ulikuwa umependwa mara moja.
MOJA KATI YA WIMBO WA CHAKACHAKA MAMALAND NAUPENDA SANA
Nyimbo kama "I'm Burning Up", "I Cry for Freedom", "Makoti", "Motherland" na iliyopendwa, "Umqombothi" mara moja zilihakikisha hali ya Chaka Chaka's sasa kama nyota kwenye sekta ya muziki huko Afrika ya Kusini. Chaka Chaka alikulia katika maisha ya  shida akilelewa na Baba yake  ambaye alifariki alipokuwa na miaka 11 na mama yake alikuwa ni  mfanyakazi wa nyumbani, aliwalea mabinti watatu kwa mshahara wake duni wa 40Rand.
Ana shahada mbili kutoka Chuo Kikuu cha Afrika ya Kusini, moja katika elimu ya watu wazima, nyingine katika serikali, usimamizi na utawala. Pia alisoma hotuba na kuigiza katika Trinity College, London, akihitimu mwaka 1997.
AFRICAN WOMEN YVONNE CHAKA CHAKA

Chaka Chaka anamiliki kampuni na gari aina za Limousine pamoja na mume wake, Dk Mandlalele Mhinga, ana studio yake mwenyewe Halisi na kampuni yake ya kubuni ngoma mwenyewe. Anafundisha mara nyingine kusoma katika Chuo Kikuu cha Afrika ya Kusini, yupo katika bodi ya mashirika ya hisani na Mashirika yasiyokuwa ya serikali, na ni mtumishi kwenye bodi la Kampuni ya Utalii ya Johannesburg.

Jumatano, Julai 18, 2012

NYOTA WA LEO NELSON MANDELA HAPPY BIRTHDAY MADIBA

Leo Jumatano, 18 Julai ni kumbukumbu ya kuzaliwa Mzee Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini ya Kidemokrasia (18.07.1918). Kadri ya kumbukumbu zangu huyu ndiye mtu pekee ambaye Umoja wa Mataifa umemtengea siku katika mwaka mahususi kwa heshima yake. Hivi leo anatimiza miaka 94 toka azaliwe; ni mmoja kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameishi kwa muda mrefu.


Nelson Mandela ni mtu anayepewa heshima kubwa duniani kote kwa wanaomfahamu na hata wasiomfahamu. Watu wengi hasa nje ya Afrika hususani katika jamii zinazopenda kusoma vitabu wanamfahamu kupitia kitabu chake cha "Long Walk to Freedom". Hiki ni kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake kwa kina kabisa. Sehemu kubwa ya kitabu hicho ameandika yeye mwenyewe na tena akiwa gerezani. Hili ni moja ya mambo ya kujifunza toka kwa mzee huyu-maktaba kubwa duniani kote. Tujipange tuandike historia zetu sahihi ili kuiachia jamii na dunia kwa ujumla utajiri wa mawazo kama alivyofanya mzee Mandela. Wengine tulimfahamu mzee Madiba toka enzi za utoto; tukiwa shule ya msingi tuliimba nyimbo za kutaka Mandela aachiwe huru na serikali ya makaburu. Utawala wa makabulu ulitawala Afrika Kusini kwa mabavu na kwa misingi ya kibaguzi ya rangi za binadamu; ni udhalimu wa aina yake kwa ustawi wa wanadamu


Kwanini mzee huyu ni maarufu?


Kwa hakika sifahamu yote juu ya mzee huyu anayependwa mno si tu kwake huko Afrika Kusini bali pia duniani kote kwa ujumla, hilo ladhihirika kwa Umoja wa Mataifa (UM) kumtengea siku maalum ya kumuenzi.
Mandela, alifungwa katika magereza tofauti kwa jumla ya miaka 27; umri wa kijana aliyekomaa. Mwanasiasa huyo, ambaye alikuwa pia Mwanasheria, mwanamichezo na mpigania haki za watu, alifungwa na serikali ya Makaburu kwa walichokiita uhaini. Nelson Mandela moja ya vijana walionzisha madai ya uhuru kwa njia ya mapigano alikuwa na imani kuu juu ya haki sawa kwa watu wote. Aliamini na anaamini kuwa binadamu wote ni sawa katika misingi ya ubinadamu- kwa haki na mahitaji yetu. Ni kwa imani na msukumo huo wa kudai uhuru na haki za watu wote wa Afrika Kusini ndo alikuwa tayari kudai haki hizo hata kama ingemlazimu kuyatoa maisha yake; funzo kubwa hilo.



 Kwa hakika imani juu ya haki sawa kwa watu wote ni funzo na changamoto kubwa kwa viongozi wote duniani. Nini imani yako wewe kiongozi juu ya haki sawa kwa wananchi unaowaongoza? Ni dhahiri kuwa unatambua kuwa wananchi wako wote wanahitaji chakula cha kutosha, makazi, huduma muhimu za kijamii; afya, elimu, na kadhalika (nk). Lakini tunacho kishuhudia hii leo ni ubinafsi mkubwa wa viongo na hata wananchi wengine wenye nafasi bila kujali mahitaji ya wengine wenye haja ya vile vitu tu vya msingi. Wasomi wengi katika nchi zetu zinazoendelea tunahangaika na mahitaji ya ziada ila hali kuna wenzetu wengi tu wasio na mahitaji yao ya lazima. Tukitaka kutambulika vyema hapa duniani ni lazima tujifunze kwa mzee Mandela kujisahamu kwa ajili ya wengine.
Suala kuu ambalo dunia imejifunza toka kwa mzee huyu wa miaka 94 sasa ni moyo wa msamaha. Kumbe hata kwa binadamu msamaha unawezekana. Msamaha huu umeongozwa na busara kuu bila shaka na neema tele za Mwenyezi Mungu. Rais Nelson Mandela angeweza kabisa kulipa kisasi cha Waafrika Kusini weusi wengi waliopoteza maisha kwenye harakati za kujikomboa, lakini hakufanya hivyo, alisamehe na badala yake aliwaunganisha wananchi wote wa Afrika Kusini mpya, ingawa kuna vidonda vingi na makovu watakayoishi nayo daima, na kuanza kuijenga nchi yao kwa manufaa yao wote. Hii ni changamoto kuu kwa wanadamu wote - nadhani ni sababu hii hasa ndo imeulazimu Umoja wa Mataifa kuanzisha siku mahususi kumuenzi mpigania haki za binadamu Nelson Mandela Madiba. Kwa hakika Madiba ni mjenga dunia!!!
IMEANDIKWA NA  http://francisgodwin.blogspot.com/

Jumatatu, Julai 09, 2012

"MAPENZI HAYAANGALII UMRI" NYOTA WA LEO MARIAH CAREY

Mariah Carey (amezaliwa tar. 27 Machi, 1970) ni mwanamuziki, mtunzi, mtayarishaji na pia ni mwigizaji wa Kimarekani. Alitengeneza albamu yake iliyofanya vizuri katika masoko mbalimbali na chati mbalimbali mwaka 1990, chini ya studio ya Columbia Records chini ya Tommy Mottola na kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kufikisha wimbo katika nafasi ya kwanza nchini Marekani. 

Mariah  mwenye umri wa miaka 42  na Muigizaji  Nick Cannon, mwenye umri wa miaka 31 walifunga ndoa Aprili   30, 2007 nchini Bahamas. Carey na Cannon walipata watoto mapacha wao wa kwanza  wa kike anaitwa Manroe na wa kiume anaitwa Moroccan April 30, 2011 katika hospitali ya  Los Angeles

Tofauti kubwa ya umri iliyopo baina yao imekuwa ikizua maneno  tangu wawili hao walipooana wengine wamekuwa wakimshutumu kijana huyo kuwa amefuata mali kwa mwanamama huyo mwenye utajiri mkubwa unaokadiriwa kuzido dola milioni 225 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 300 ambazo zimemfanya atese mara kwa mara katika chati za wanamuziki wa kike matajiri zaidi duniani. 

Maneno ya watu kuhusiana na uhusiano wao hazionyeshi kuteteresha uhusiano wao  kwani bado wanaendelea kufurahia ndoa yao. Mariah  Carely ndoa yake ya kwanza alifunga na mmiliki wa lebo ya kurekodi  muziki ya Sonny Tommy Mottola mara kwa mara amelazimika kukanusha mahusiano na rapa mtukutu  Eminem ambaye amekuwa akidai kuwa waliwahi kuwa wapenzi

Malumbano ya Eminem na Mariah yaliendela hadi  kuamua  kuandika wimbo wa kumponda mwenzake  wimbo unaoitwa OBSSSED ambapo katika video yake anatokea kijana anayevaa OPP, kama Eminem akimfuata fuata Mariah kila aendako. Cannon naye alishawahi kusema kwamba atamfanyia kitu Mbaya rapa Eminnem ambaye jina lake halisi ni Marshall Mathers.

Mariah na Cannon siku ya ndoa yao haijalishi umri hapa ni mapenzi tu 

Jumatano, Juni 20, 2012

NYOTA WA LEO CHRIS BROWN

Christopher Maurice "Chris" Brown (amezaliwa tar. 5 Mei, 1989) ni msanii wa muziki na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Ameanza kutoa rekodi yake ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2005 yenye jina sawa na lake, yaani, Chris Brown akiwa na umri wa miaka 16. Albamu ina kibao kikali cha "Run It!", ambacho kilifikia nafasi ya juu kwenye Billboard Hot .


Licha ya kupata mafanikio makubwa akiwa kama msanii wa kujitegemea, Brown amepata kushirikishwa kwenye vibao vingine vikali kama vile "No Air", aliimba pamoja na Jordin Sparks, "Shortie like Mine" sambamba kabisa na rapa Bow Wow na "Shawty Get Loose" na Lil Mama na T-Pain. Kibao hicho kilishika nafasi ya tatu, namba tisa na kumi kwenye chati za Billboard Hot 100 mfululizo


Kutokana na utaratibu wake wa kucheza, Brown amefananishwa na wasanii kama vile Usher na Michael Jackson,

Mnamo 2009, Brown alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mwandani wake - mwimbaji Rihanna, na akapigwa kifungo cha nje cha miaka mitano na miezi sita
Tetesi za hivi karibuni ni kwamba Rihanna na Chris Brown waamerudiana na hata kupelekea ugomvi baina ya Drake na Chris Brown uliosababishwa na wivu wa kimapenzi hadi kutupiana vyupa.

Jumatano, Mei 09, 2012

NYOTA WA LEO

Beyoncé Giselle Knowles alizaliwa tarehe 4 Septemba, 1981), anayefahamika zaidi kwa jina moja Beyoncé ni mwimbaji wa R & B, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji na mwanamitindo kutoka Marekani. Alizaliwa na kukulia Houston, Texas na alihudhuria shule mbalimbali zinazofunza sanaa. Pia alianza kushiriki katika mashindano ya kuimba na kucheza ngoma akiwa mtoto. Knowles alikuja kujulikana katika mwisho wa miaka ya 1990 kama mwimbaji kiongozi wa kikundi cha wasichana cha R & B, Destiny's Child

Beyonce akiwa na mtoto wake Blue Ivy Carter

Wakati wa kuvunjika kwa kikundi cha Destiny's Child, Knowles alitoa albamu yake ya kwanza, Dangerously in Love (2003), ambayo ilikuwa mojawapo ya albamu za mwaka zilizokuwa na mafanikio zaidi na jambo hili liliashiria uwezo wake wa kufaulu kama msanii kivyake. Albamu hiyo ilikuwa na mafanikio muhimu ya kibiashara, huku ikitoa nyimbo mashuhuri kama "Crazy in Love", "Baby Boy", na kumshindia Knowles tuzo tano za Grammy katika mwaka 2004

cute one

Muonekano wa Beyonce Baada ya kupata mtoto
LOVELY COUPLE BEYONCE AND JAY Z

Beyonce ni msanii ambaye anafanya juhudi sana katika kazi zake moja kati ya nyimbo zake ninazozipenda unaitwa WHO RUN THE WORLD

Jumatano, Aprili 25, 2012

NYOTA WA LEO

Brandy Rayana Norwood (amezaliwa 11 Februari 1979) ni mwimbaji kutoka nchi ya Marekani

Akiwa na rafiki yake Monica Arnold  waliwahi kufanya vizuri sana na single ya THE BOY IS MINE

Akiwa na mdogo wake anayeitwa Ray J ambaye pia ni msanii



Nimependa kukuwekea picha zake mbalimbali navutiwa sana na sauti yake nyororo katika wimbo wa PIANO,LONG DISTANCE,RIGHT HERE na nyngine nyingi

Kutokana na sauti yake kuwa nzuri Brandy amejipatia umaarufu mkubwa kama Princess of RNB

Brandy akiwa shoping na mtoto wake  anayeitwa  Sy'ray

Ijumaa, Aprili 06, 2012

Nyota wa leo Michelle Obama

Michelle LaVaughn Obama (jina la kuzaliwa ni Michelle LaVaughn Robinson), amezaliwa mnamo tar. 17 Januari, 1964) ni Mwanasheria wa Kimarekani na ndiyo mke wa Rais wa Marekani Bw. Barack Obama. Huyu ndiye Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani.

Michelle alizaliwa na kukulia kitongoji South Side ya Chicago na kusoma hadi kuelekea katika Chuo Kikuu cha Princeton halafu baadaye katika Kitivo cha Sheria cha Harvard.Baada ya kumaliza elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika kampuni ya Sidley Austin, halafu baadaye akaja kuwa kama mmoja kati ya wafanyakazi wa meya wa Chicago Bw. Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Chicago na Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.



Michelle Obama ni dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University. Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini Chicago South Side kuliko kuishi mjini Washington, D.C.

FIRST LADY
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom