Jumanne, Machi 26, 2013

NYOTA WA LEO CHINUA ACHEBE, AMEACHA PENGO KUBWA KATIKA FASIHI. TUTAMKUMBUKA MILELE KWA UWEZO WAKE WA KUANDIKA VITU VINAVYOGUSA JAMII

Aliandika kitabu chake ‘Things Fall Apart’ katika miaka ya 20 kikielezea jinsi wazee wa kikabila wa Nigeria walivyosalimu amri mbele ya  wakoloni wa Uingereza.Kitabu hicho kimetafsriwa katika  lugha zaidi ya 50 na kuuza nakala milioni 8 kote duniani.
Achebe alipooza kutokana na ajali ya barabarani  mwaka wa 1990 na ameishi Marekani kwa miaka mingi tangu wakati huo, akiendelea kutetea demokrasia katika nchi yake asili ya Nigeria.

Baada ya Achebe kuingia chuo kikuu, alipenda zaidi kusoma kazi za wanafasihi wengine, lakini pia alipendelea kuandika hadithi mbalimbali na alipomaliza masomo chuo kikuu aliajiriwa katika kituo cha utangazaji Nigeria NBS.

Alijaribu kuingia katika vyama vya siasa mwaka 1970 lakini aliacha baada ya kushuhudia rushwa na uvunjaji wa sheria uliokithiri.September 1961 Achebe alifunga ndoa na Christine Okeli mfanyakazi mwenzake katika television ya NBS. Walibahatika kupata watoto wanne na ndoa yao inatajwa kuwa yenye amani na upendo thabiti.
Chinua Achebe’s family, his wife Christie (in red), his youngest daughter Nwando and sons Ikechukwu and Chidi (in black).
 

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom