“Napata maumivu makali sana jamani naombeni mnisaidie
nateseka sana eeh Mungu wangu” ilikuwa ni sauti ya Mama kutoka chumbani niliinuka na kukimbilia
ndani huku nikimwangalia Mama kwa huzuni kutokana na maumivu ya tumbo aliyokuwa
akiyasikia nilisogea karibu “Pole mama twende nikupeleke Hospitali” Alijivuta
kidogo na kuinua uso wake huku akinitazama “Mwanangu baba yako yuko wapi” Nilimshika mama mkono “Baba ametoka ameenda
kazini”.
Kutokana na hali aliyokuwa nayo Mama nilitamani kumsaidia lakini sikuwa
na namna kwani maumivu aliyokuwa anayapata yalikuwa makali sana “Kandida
mwanangu naomba umtafute Baba yako anipeleke hospitalini” Baba yangu
alikuwa ni mfanyakazi katika kiwanda cha plastiki na Mama alikuwa hana kazi
nikiwa ni mtoto wa kwanza katika familia yetu na wadogo zangu wawili ambao wote
walikuwa wakisoma shule ya msingi wakati huo mimi nilikuwa kidato cha pili pale
nyumbani hakukuwa na mtu yeyote zaidi yangu na Mama alikuwa ni mgonjwa, hali ya
mama yangu ilizidi kuwa mbaya ikanibidi nikimbie kwenda kumuita jirani yetu
anayeitwa Mama Keku.
“Mama keku ,Mama
keku” Niliita kwa sauti kubwa iliyojaa wasiwasi mwingi “hee kuna nini
Kandida mbona unaita kwa sauti kali hivyo” Alinijibu mama
keku huku akitoka chumbani kwake wakati
huo machozi yalikuwa yakinibubujika kwa wingi “Mama yangu anaumwa, Mama yangu
anakufa jamani naomba uje umsaidie tumpeleke hospitali” Niliongea kama
nimechanganyikiwa.
“Sasa mbona
sikuelewi, inamaana amezidiwa yuko
na nani nyumbani? Embu twende haraka ukilia haisadii chochote” Tuliondoka haraka
nyumbani kwa Mama Keku na kuelekea chumbani kwa mama yangu safari hii tulimkuta Mama akiwa kimya huku macho yakiwa yamemjaa machozi na hata tulipomuita hakuzungumza
lolote “Mama yangu jamani Mama uwiiiiiii nisaidie mimi Mama yangu” Nililia kwa
uchungu nikijua Mama yangu atakuwa amefariki Mama Keku alitoka nje haraka
kwaajili ya kwenda kutafuta usafiri wa kumpeleka Mama hospitali .
Alirudi akiwa na
usafiri wa gari dogo taksi aina ya corolla na majirani walisaidiana kumbeba mama na
kumpeleka hospitalini.kulikuwa na umbali mkubwa sana hadi kufika katika
hospitalini tulipofika pale wahudumu walikuja na kitanda cha kuwabebea
wagonjwa (machela) na kumbeba mama
haraka kumpeleka kwa daktari kwa uchunguzi zaidi Mama keku alimpigia simu Baba na kumjulisha kuwa tulikuwa Hospitalini
na hali ya mama Ni mbaya Baba alifanya haraka ili kufika pale hospitalini.
Ilipita
kama nusu saa tokea mama aingizwe katika chumba cha uchunguzi Daktari alikuja
“anayehusika na mgonjwa ni nani?” aliuliza huku mimi na mama keku tukiwa
tunamsikiliza “Mimi ndiye niliyemleta mgonjwa ni jirani yangu na huyu hapa ni
mtoto wake” alisema Mama Keku “Hakuna ndugu mwingine wa karibu zaidi ” aliuliza
Daktari “Mume wake yupo njiani anakuja alijibu mama Keku “Akifika mwambie aje anione “Mama yangu
anaendeleaje naomba kumuona” Nilimsogelea Daktari na kumshika katika
koti lake kwa nguvu kwani nilikuwa kama nimechanganyikiwa sijui nini hatima ya Mama yangu “Usijali mtoto tulia Mama yako
anaendelea na matibabu utapata nafasi ya kumuona baadaye. Nini kitaendelea usikose SURA YA PILI......................
|
Maoni 7 :
Inaendelea lini tena dia
Mwanzo mzuri, ila imekuwa fupi xna ktk kipande hicho cha kwanza. Tupia, tupia kitu watu wajifunze ya dunia.
iko pouwa ile mbaya
asanteni sana wadau tuko pamoja sana
Nice na Hongera
Nice na Hongera sana
Adela, mbona kama ile hadithi ya chungu na tamu ya penzi haijaisha au kuna vipande ambavyo sijaona, maana naona similizi ya mwisho nimeisikiliza imeishia yule dada anapanga kutoroshwa kesho yake arudi Dar baada ya kugundua ngereza ni mchawi, then ikakatika, najaribu kutafuta muendelezo wake sioni. Asante dear simulizi zako ni nzuri sana.
Chapisha Maoni