Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo AFYA NA UREMBO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo AFYA NA UREMBO. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, Mei 19, 2014

MADHARA YA MWANAMKE KUZAA MFULULIZO BILA KUPUMZIKA.

Ni wazi vifo vya  uzazi  vimekuwa vikisababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya mwanamke kuzaa mfululizo bila kupumzika hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja kwa wakuu wa mikoa ya kanda ya magharibi, kanda ya ziwa na kwingineko kuongeza juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi wake umuhimu wa kutumia njia ya uzazi wa mpango.

Wakuu hao wana kazi ya kuondoa mila na desturi za wananchi wa ukanda huo ili waondokane na mila hizo zilizopitwa na wakati kwa kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango katika kuwezesha taifa kukua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi, Takwimu za nchi zinaonyesha kanda ya magharibi inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kuzaana na kufikiwa asilimia 7.1 ikifuatiwa na kanda ya ya kati na kufuatiwa na kanda ya ziwa hali hii pia inachangia ongezeko la vifo vya uzazi kwa wanawake kutopumzika. Kuna haja wananchi kuelimishwa kuwa matumizi mazuri ya njia ya uzazi hayana madhara mwilini ili waweze kuzaa kwa mpango na kupunguza vifo vya uzazi.
 Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alizindua mpango mkakati ulioboreshwa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuwataka watendaji wake katika mikoa yote nchini, ambao ni wakuu wa mikoa kuwa wahakikishe wanapunguza vifo vya watoto na akinamama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi.

Ijumaa, Januari 31, 2014

CHONDE CHONDE ULEVI WAONGEZA SARATANI YA NGOZI KWA ASILIMIA 50

Unywaji wa pombe kwa wingi unadaiwa kusababisha saratani ya ngozi aina ya milanoma, Watu wanaokunywa  chupa moja ya pombe kwa siku wana hatari kwa asilimia 10 ya kupata aina hiyo ya saratani ukilinganisha na wale wanaokunywa mara mojamoja

Wanaokunywa chupa mbili kila siku wana hatari kwa asilimia 18 ya kupata saratani hiyo ya ngozi ambayo inawaathiri zaidi vijana.Wanywaji sugu ambao hunywa glasi  nne kila siku, wapo katika  hatari kwa asilimia 55 kutokana na taarifa za kimataifa za watafiti. Chupa moja ya pombe ina gramu 12.5 ya kilevi ambayo inatajwa kusababisha mabadiliko ya kibiolojia na kuifanya ngozi  kuathirika kwa urahisi na jua.

Haijafahamika moja kwa moja ni kwa namna gani pombe inachochea saratani lakini watafiti hao wanaamini kuwa ethanol ikibadilika na kuwa kemikali huweza kuchangia kuongezeka kwa saratani hiyo.

Jumatatu, Januari 06, 2014

WASEMAVYO WATAALAMU SI VYEMA WANAWAKE WAJAWAZITO KUVAA VIATU VIREFU NA TOP ZA KUBANA

Iwapo mwanamke atapendelea kuvaa viatu virefu au nguo za kubana kipindi cha ujauzito.Matatizo ya kuumwa miguu, kiuno mgongo ni rahisi kumpata. Visigino virefu  hubadili miundo ya miguu,hivyo hupelekea magoti na mapja kufanya kazi ya ziada ili kuupa mwili usawa kwakuwa misuli inafanya kazi kubwa.Huwezekano wa kupatwa na matatizo ya kuumwa miguu na kushindwa kutembea siku za baadaye ni mkubwa zaidi.
Viatu virefu, husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya miguu,neva ya fahamu kushindwa kufanya kazi vizuri na matatizo kwenye nyonga.Bora na wale wanaovaa kwa muda mchache , sasa mwingine unakuta anatembea mwendo mrefu halafu anakazana na viatu virefu (high heels)  ni bora kuwa huru kwa kuvaa kiatu kulingana na mazingira unayokwenda.

Jumamosi, Novemba 23, 2013

TAHADHARI KWA KINA MAMA WANAOPENDA KUTUMIA KILEVI NA KUVUTA SIGARA WAKATI WA UJAUZITO

Utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya katika sehemu mbalimbali unaonyesha kuwa pombe ina athari kubwa na mbaya hasa kwa kina mama wajawazito na matatizo wanayoyapata yanafahamika kitaalamu Fetal Alcoholic Syndrome (FAS). Watoto wengi wanaozaliwa na tatizo hili  wanakuwa na nyuso ambazo siyo za kawaida,  (fasial deformities). Watoto hawa wanaweza kuwa na pua  bapa na macho yaliyoingia ndani au kupata matatizo ya kusikia  na kutokuwa na uwezo wa kusoma.

Na wataalamu wanasema  ni vigumu kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili na mara nyingi ni kwa watoto kabla ya kutimiza miaka kati ya mitatu na minne. Dalili zinazoonyesha mtoto ana tatizo hili ni kwanza haonyeshi dalili ya kulia au anaweza kulia kwa kiasi kidogo, huchelewa kutembea na hata kuongea, haonyeshi kuvutiwa na mazingira yanayomzunguka yaani hata kama kuna vitu vya kucheza hapendi kujishughulisha navyo.Ukiona dalili hizi nenda kituo cha afya.

NI MUHIMU  KUACHA MARA MOJA ILI KUMUEPUSHA MTOTO NA MATATIZO AMBAYO YANAWEZA KUMLETEA MADHRA MAKUBWA KATIKA AFYA YAKE.

Jumapili, Septemba 22, 2013

UKIWA UNAWEKA DAWA YA EASY WAVES KWA NYWELE FUPI HAYA NI MAFUTA MAZURI KWA MUONEKANO MZURI WA NYWELE ZAKO

 Baada ya kuosha nywele zako vizuri, kwanza inakubidi upake pink lotion ili zibaki kuwa laini na baada ya kukauka vizuri basi unachukua mafuta ya nywele  ya mgando yoyote ambayo ungependelea kupaka, kabla ya kupaka hii gel activator.

Ukishapaka kiasi kidogo cha mafuta basi unachukua Sofnfree yako unapakaa vizuri kabisa hadi inakolea nywele zinakuwa katika mwonekano mzuri zaidi binafsi  mimi ndivyo ninavyofanya. jambo la muhimu hakikisha unapakaa pink lotion na mafuta mengine ya nywele ya kawaida unayotumia kwa kiasi kidogo halafu ndiyo unamalizia na hii gel activator.

NA NYWELE ZAKO ZINAKUWA NA AFYA NA KUPENDEZA WAKATI WOTE.

Alhamisi, Septemba 05, 2013

PENDELEA KUNYWA JUICE YA KUTENGENEZA MWENYEWE

Juice ya kutengeneza mwenyewe ni nzuri zaidi, ikiwa ni kwa matunda ya aina mbalimbali, kama maembe, machungwa, tikiti maji, nanasi nk, Juice unaweza kunywa wakati wowote ule, unaweza kuifanya kama kifungua kinywa, badala ya kunywa chai au maziwa asubuhi unakunywa juice ni nzuri pia kwa wale wanaopenda kupunguza uzito, kwani unapotengeneza juice yako kwa mchanganyiko wa matunda bila ya kuweka sukari basi inasaidia sana kupunguza mafuta mwilini. 

Jumapili, Agosti 25, 2013

PENDELEA KULA BAMIA UPATE FAIDA ZAKE

 Bamia inafahamika kwa wengi  katika jamii kwa ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo.
Wapo wanaoitumia kama kiungo cha mboga na wengine huifanya mboga kamili.
Bamia ina majina lukuki, wengine huiita okra, kwa jina lisilo rasmi la Kiingereza huitwa, ‘lady finger’ au gumbo.
Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kisayansi huitwa, ‘Abelmoschus Esculentus’
Kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo mikoa mikavu kama Dodoma, Singida katika Tanzania.
Kwa kawaida huwa na rangi ya kijani iliyokolea na hukua hadi kuwa na urefu wa sentimeta tano hadi 15.

 
 Zijue faida za bamia kiafya:
Bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Kwa kifupi,  sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake.
Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi.  Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara kutaimairisha mwanga katika macho yako.
Wingi wa vitamini A huzuia maradhi  yatokanayo na virusi kama mafua.

Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi.
Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo.  Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Jumatatu, Agosti 05, 2013

KIBOKO YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI BILA MADHARA

UKITUMIA  MRT COMPLEX ni njia pekee inayotoa mafuta yasiyohitajika mwilini na kurudisha chembechembe hai. Ni nzuri kwa watu wenye magonjwa ya kisukari, moyo, kiharusi, shinikizo la damu na figo.. Huongeza virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika kuboresha na kuupa mwili nguvu. Tumia bidhaa za edmark. NI MUHIMU KUISHI MAISHA MAZURI YENYE AFYA BORA. WASILIANA NA BWANA William kwa namba 0713258053 au 0769 258053. au email kavisheadela@yahoo.com

Jumatano, Julai 24, 2013

VIAZI VITAMU VINAWEZA KUWA MOJA KATI YA CHAKULA KATIKA FUTARI YAKO.

Ni ukweli ulio wazi kuwa, njia bora na ya kipekee ya kukabiliana na ukosefu wa kinga mwilini, ni kula mlo wenye virutubisho vyote muhimu. Hivyo, inashauriwa mlo wako uwe kwa kiasi kikubwa ni wa vitu vifutavyo:

Hakikisha unakula kwa wingi matunda, mboga za majani, nafaka lishe, maharage na karanga, epuka kula kwa wingi sukari, hasa nyeupe. Pia kula vyakula kwa wingi kama machungwa, karoti, viazi vitamu, nyanya na pilipili mboga bila kusahau jamii zote za kabichi.

Unaweza kupika viazi vitamu kwa kuchemsha tu, au kuviunga  pamoja na nazi.Viazi vitamu ni chakula kizuri kwa  gharama nafuu pia.

Alhamisi, Julai 18, 2013

FUTARI YAKO IENDE SAMBAMBA NA MATUNDA PAMOJA NA MBOGAMBOGA


Inapendeza kula matunda mara kwa mara kwani unaambiwa usisubiri kupata ushauri wa Daktari ndiyo  ule matunda. Siku zote hakikisha mbogamboga na matunda inakuwa sehemu  ya mlo wako wa kila siku.

Jumanne, Julai 16, 2013

TUMIA SPLINA LIQUID CHLOROPHYLL NA KUWEKA MWILI WAKO KATIKA HALI YA USAWA UNAOTAKIWA .

Ni nzuri sana ikitumiwa na watu wenye kusumbuliwa na vidonda vya tumbo, pia wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari, saratani, moyo, shinikizo la damu, pumu, kikohozi, mafua ya mara kwa mara, mzia vidonda, vipele na harara, majipu na malaria  pia husawazisha kiwango cha acid- alkaline na kuweka mwili wako katika hali ya usawa unaotakiwa. Kwa atakayehitaji tunaweza kuwasiliana kwa maelekezo zaidi. kavisheadela@yahoo.com
MUHIMU KUISHI MAISHA MAZURI NA YENYE AFYA BORA. TUMIA BIDHAA  ZA EDMARK. 

Ijumaa, Mei 17, 2013

KUWA MAKINI KATIKA ULAJI WA VYAKULA. NI MUHIMU KUISHI MAISHA MAZURI NA YENYE AFYA BORA

kwa kiasi kikubwa chakula kinachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Hivyo ni vyema kuwa na mpangilio mzuri wa vyakula kwani chakula kinapotumika vibaya kinaleta athari kubwa sana kiafya na hata kifo.. Ili kuepukana na atahari hizo ni vyema kula chakula kizuri kama mbogamboga,mihogo pamoja na jamii ya maharagwe na matunda kwa wingi epuka kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

Kuna uwezekano wa kupata maradhi kama saratani ya utumbo mkubwa, vidonda vya tumbo, shinikizo la damu, kisukari matatizo ya moyo nk. kutokana  na kutokuwa na mpangilio mzuri wa vyakula .Sababu kubwa ya matokeo hayo ni kutokufanya kazi vizuri kwa mfumo mzima wa usagaji wa chakula . NI VYEMA KUWA MAKINI NA VYAKULA TUNAVYOKULA KILA SIKU. mfano chipsi usiwe ndiyo mlo wako mkubwa, piza nk.Unaweza kuepukana na matatizo haya kwa kupata ushauri wa daktari pamoja na kutumia bidhaa za Edmark 
DAWA HII INASAIDIA KUTOA  MAFUTA YASIYOHITAJIKA MWILINI NA KURUDISHA CHEMBECHEMBE  HAI. NI NZURI SANA KWA WATU WENYE MAGONJWA YA KISUKARI,FIGO, MOYO PAMOJA NA SHINIKIZO LA DAMU.

Alhamisi, Mei 09, 2013

PENDELEA KULA MACHUNGWA UPATE FAIDA ZAKE

UKOSEFU WA CHOO
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

2.UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!

3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

4. UGONJWA WA MAPAFU
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.

5. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.

6. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.

7. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.

8. UKUAJI WA UBONGO
Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.

9. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.

10. UGONJWA WA FIGO
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.

11. VIDONDA VYA TUMBO
Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.

12. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.

13. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida h

6. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.

Jumatatu, Aprili 29, 2013

PENDELEA KULA NDIZI UPATE FAIDA ZAKE

  Ndizi ni aina ya tunda linalopendwa na watu wengi yawezekana huwa unakula tunda hili bila kujua faida zake, lakini pia yawezekana wewe hupendi kabisa kula ndizi mbivu, lakini ni vyema kufahamu kuwa tunda hili ni muhimu sana kwa afya yako inasaidia kama wewe hujapatwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi kuhusu tunda hili, ndizi ni chanzo kikubwa cha madini aina ya ‘Potassium’, ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na huboresha utendajikazi mzuri wa moyo. Ndizi moja tu kwa siku inaweza kukukinga na maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

Jumatatu, Machi 18, 2013

NI VYEMA KUBADILI MTINDO WA MAISHA KUEPUKA UGONJWA WA KISUKARI.

Kwa kupunguza kiwango cha sukari na mafuta katika milo ya kila siku, na kuacha uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi, Takwimu zinaonyesha kuwa  watu zaidi ya milioni 347 wanaugua kisukari duniani kote. Shirika la afya Duniani (WHO) limetoa onyo kwa watu duniani kote wanaweza kubadili mtindo wa maisha ili kuepukana na ugonjwa wa kisukari.  Mwaka 2004, watu zaidi ya milioni 3.4walikufa kutokana na ugonjwa hu. WHO imetabiri kuwa ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa kisukari utakuwa chanzo kikuu cha vifo duniani.

Jumanne, Februari 26, 2013

Muonekana wa rangi ya asili kwa kutumia vipodozi asilia

Natumia mafuta ya Vestiline ambayo kwa kiasi kikubwa yanasaidia kutunza ngozi yangu  lakini pia kumbuka kula matunda kama karoti mbichi, matango nk husaidia kungarisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo. Ni vyema kutambua ngozi yako ni ya aina gani kwa vipodozi sahihi wakati mwingine ni vizuri kuwauliza wataalamu kwa matumizi sahihi ya vipodozi



Jumatano, Januari 02, 2013

UNAWEZAJE KUTUNZA NYWELE ZAKO ZA ASILI??


Mimi nazipenda nywele zangu na mara nyingi nakuwa makini ili zisikatike au kudhoofika siyo gharama unaweza kutumia njia zifuatazo  Katika suala la utunzaji wa nywele haliangalii mwanamke au mwanaume ni vyema kuzipenda nywele zako za asili, Hakikisha unasafisha nywele zako mara kwa mara kwa kutumia maji ya uvuguvugu na sabuni maalum kwa ajili ya kuoshea nywele (Shampoo).Lengo la kutumia maji ya uvuguvugu ni kuondoa uchafu wote unaoganda kwenye ngozi kutokana na mafuta, hivyo ni vyema ukatumia maji hayo walau mara moja kwa wiki.


Kausha nywele kwa taulo au kitambaa kisafi mpaka uhakikishe hakuna maji kabisa yaliyobaki.Baada ya nywele kuwa kavu, paka mafuta ya kutosha kwenye nywele zako huku ukihakikisha ngozi nayo inapata mafuta kuepusha ukavu ambao mara nyingi husababisha mba.Uwepo wa mafuta husababisha  nywele kung’aa na kuvutia,waweza pia kuzichana hata kuzibana kwa mtindo wowote.  lakini pia angalizo kwa wanaoshonea  weaving mara kwa mara wapo hatarini katika kukatika kwa nywele ni vyema kuzifanya steaming kabla ya kusuka na usikae na weaving muda mrefu ni vyema wakati mwingine kubaki na nywele za asili.

Jumatatu, Desemba 03, 2012

Ulaji wa mbogamboga si lazima upate ushauri wa daktari pendelea kula mbogamboa wakati wote

Kula mbogamboga kwa afya yako 

matunda na mbogamboga ni chakula kizuri na cha asili kwa watu wote

Alhamisi, Novemba 22, 2012

PENDELEA KUNYWA MAJI MENGI ZAIDI KULIKO KILEVI AU SODA AMA JUICE

Wataalamu wanakuambia ni vyema kunywa maji kila siku walau lita nne kwa siku lakini kwa kiasi kikubwa mtu huweza kunywa soda nyingi amba kilevi cha aina fulani kwa kiasi kikubwa kuliko kunywa maji. lakini maji  ni mazuri zaidi kiafya  na pia inashauriwa unapoamka asubuhi kabla ya kusafisha kinywa kunywa  glasi nne za maji yasiwe ya baridi ni mazuri sana kwa afya na pia husaidia kulainisha choo kwa wale wenye matatizo ya tumbo .

yafanye maji kuwa kilevi chako kwani husaidia pia kunyevusha ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa laini na ya kuvutia .  Kuna watu inaweza kuisha siku nzima bila kunywa maji hata kidogo kwa kufanya hivyo unahatarisha usalama wa afya yako kwani maji yanasaidia vitu vingi mojawapo ni kusafisha mkojo na kuepukana na magonjwa kama U.T.I

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom