Ni wazi vifo vya uzazi vimekuwa vikisababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya mwanamke kuzaa mfululizo bila kupumzika hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja kwa wakuu wa mikoa ya kanda ya magharibi, kanda ya ziwa na kwingineko kuongeza juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi wake umuhimu wa kutumia njia ya uzazi wa mpango.
Wakuu hao wana kazi ya kuondoa mila na desturi za wananchi wa ukanda huo ili waondokane na mila hizo zilizopitwa na wakati kwa kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango katika kuwezesha taifa kukua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi, Takwimu za nchi zinaonyesha kanda ya magharibi inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kuzaana na kufikiwa asilimia 7.1 ikifuatiwa na kanda ya ya kati na kufuatiwa na kanda ya ziwa hali hii pia inachangia ongezeko la vifo vya uzazi kwa wanawake kutopumzika. Kuna haja wananchi kuelimishwa kuwa matumizi mazuri ya njia ya uzazi hayana madhara mwilini ili waweze kuzaa kwa mpango na kupunguza vifo vya uzazi.
Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alizindua mpango mkakati ulioboreshwa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuwataka watendaji wake katika mikoa yote nchini, ambao ni wakuu wa mikoa kuwa wahakikishe wanapunguza vifo vya watoto na akinamama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni