Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KONA YA USHAURI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KONA YA USHAURI. Onyesha machapisho yote
Jumatano, Novemba 06, 2013
Jumatatu, Mei 27, 2013
"MIMI NI MWANAUME NIMEPIMA UGONJWA WA UKIMWI NA KUJIGUNDUA KUWA NIMEATHIRIKA LAKINI NAOGOPA KUMWAMBIA MKE WANGU NAOMBENI USHAURI"
Dada Adela samahani naomba unisaidie kuomba ushauri kwa wadau wa blog yako. Mimi ni mwanaume nina umri wa miaka 38 nina mke na watoto wawili, Naipenda sana familia yangu lakini tatizo limejitokeza baada ya mimi kuwa na safiri mara kwa mara katika biashara zangu na kujikuta nikiwa mbali na familia yangu kwa muda mrefu.Wakati mwingine zaidi hata ya miezi mitano nilijikuta naanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja ambaye nilikuwa nikishiri naye tendo la ndoa bila ya kinga na pia nikirudi nyumbani nashiriki tendo na mke wangu.
Hivi majuzi nimepima ukimwi na kujigundua kuwa nimeathirika, akili yangu imekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, nina mawazo sana na pia najuta kwa yote niliyoyafanya, nashindwa nitamuelezaje mke wangu. Kwani hapa nilipo sijui kama na yeye atakuwa ameathirika au la na pia naogopa kumpoteza mke wangu naombeni mnisaidie kwa ushauri jamani kwani sijielewi hapa nilipo.
Jumapili, Machi 17, 2013
ANAOMBA USHAURI "nimeolewa tatizo ni kwamba simpendi mume wangu"
habari dada Adela, naomba unisaidie kuniwekewa ujumbe wangu kwa wadau wapate kunisaidia, email yangu kapuni tafadhali, Mimi ni msichana miaka 21, nimeolewa, tatizo ni kwamba simpendi mume wangu hata kidogo, miezi mitatu ya mwanzo nilimpenda ila alivyoniambia tu kuwa ana mtoto sikuwa tena na mapenzi naye kwani sikuwa napenda kuwa na
mwanaume mwenye mtoto maana hawa mara nyingi wanaletaga matata wanajifanya kutokuwa tena na mapenzi na wanawake waliozaa nao kabla ya ndoa lakini wanawarudia, sasa nimevumilia mpaka nimechoka najilazimisha lakin yaani moyo wangu umekataa kabisa na nimezaa naye mtoto mmoja, natamani kuachana nae lakini wazazi hawakubaliani na hili, naombeni
ushauri nifanyeje? Asanteni
Alhamisi, Machi 14, 2013
"Anadai mtoto wakati hakutoa matunzo"
Jumatatu, Novemba 19, 2012
"MKE WANGU ALINIFUMANIA NIKAHISI AMENISAMEHE KUMBE LENGO LAKE NI KULIPIZA KISASI"
Habari yako Adela mimi ni mwanamume nina mke na watoto watatu tumeishi kwenye ndoa takribani miaka kumi sasa kuna kipindi mke wangu alinifumania nikiwa na mwanamke mwingine ni siku ambayo siwezi kuisahau kwani nilikuwa sina cha kujitetea ilinibidi nikubali nakuomba msamaha kwa kilichotokea huku nikiwa na nia ya kubadilika na kutorudia kosa.
Mke wangu alinisamehe lakini sikujua kumbe alikuwa na kinyongo moyoni mwake hivi majuzi nilimfumania kwenye ujumbe mfupi akiwa anawasiliana na mwanaume mwingine ikionyesha kabisa wana mahusiano ya kimapenzi ukweli ni kwamba iiliniuma sana bado kidogo nimpige nilimuuliza kwa vitisho akaniambia ameamua kufanya hivyo kwasababu na mimi nilimsaliti kitendo hiki kimeniumiza hadi natamani kumfukuza nyumbani kwangu amenikera sana sina amani.
Jumatano, Oktoba 24, 2012
"MKE WANGU ANANIKERA NA TABIA YAKE YA KUSHIRIKI KILA KITCHEN PARTY INAYOTOKEA MTAANI HATA ZA WATU AMBAO HAWAJUI"
Mimi ni mwanamume nina mke na watoto watatu, naipenda sana familia yangu lakini tatizo lipo kwa mke wangu anapenda sana kuhudhuria katika sherehe mbalimbali hakuna sherehe itakayompita kiasi kwamba naona hata kazi anashindwa kufanya inawezekana kila siku yupo kwenye vikao vya kitchen party mara harusi yaani tokea nimemuoa hii tabia imeanza ina mwaka mmoja nimeshawahi kumkalisha chini na kumshauri lakini naona tabia hiyo inaendelea inanikera sana kwani naona hana muda hata wa kukaa na watoto zaidi ya kuwaza sherehe yaani natoa michango ya hizo sherehe majina mengine siyajui ila yeye ananiletea kadi yakutaka mchango nimechoshwa na hii tabia NAOMBENI USHAURI JAMANI. Kwani amekua akitoka kwenda kwenye sherehe kila weekend na kurudi usiku wa manane.
Jumatano, Julai 11, 2012
NAHISI MKE WANGU BADO ANA MAHUSIANO NA MCHUMBA WAKE WA ZAMANI.
Mimi ni mwanamume ninaishi na mke wangu ambaye kwa sasa tuna takribani miezi nane tokea tulipofunga ndoa nampenda sana mke wangu lakini tatizo ni tabia ya mke wangu kila tunapozungumza lazima atamtaja alyekuwa mchumba wake wa zamani tena mambo mengi anayozungumza ni ya kumsifia nilishawahi kumuambia kuwa tabia yake hiyo siipendi lakini anabaki kucheka na kusema kuwa nina wivu.
Tuliendelea kuishi hivyohivyo nikaanza kufuatilia simu yake ndipo nilipokutana na ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa huyo mchumba wake wa zamani naumia sana moyoni mwangu na pia napata hasira sana kwani mpaka sasa sijamuuliza chochote nahisi kutokana na hasira nilizonazo naweza kumuumiza sijui nifanyeje katika hili NAOMBENI USHAURI
Ijumaa, Mei 04, 2012
Mke wangu ananikera na tabia ya kunisemea kwa marafiki zangu
Habari Adela mimi ni mdau wa Blog yako na hongera sana kwa kuelimisha jamii kupitia simulizi zako nzuri mimi nina tatizo naomba uniwekee kwenye blog yako nipate ushauri, Nina mke na watoto wawili familia yangu ninaipenda sana lakini tatizo ni mke wangu yaani nikichelewa kurudi nyumbani ikiwa ni katika kazi zangu za kila siku au matatizo yoyote yanayotuhusu sisi wawili anaenda kuwaambia marafiki zangu huku akisema mimi sijatulia, na niliwahi kumkalisha chini na kumuambia sipendi anavyoenda kuwaambia maneno marafiki zangu ni bora anieleze mimi mwenyewe lakini naona tabia hiyo bado inaendelea hivi majuzi ndiyo nilikereka zaidi rafiki yangu alikuja akaniambia kuwa jitahidi umridhishe mke wako mnamo sita kwa sita analalamika sana,,, niliumia sana moyoni na kujiuliza huyu mwanamke hadi mambo ya chumbani anatoa nje yaani nikipita mtaani marafiki zake wananijua kila kitu na marafiki zangu hivyohivyo hii tabia imenichosha wakati mwingine najuta kwanini nilimuoa
Jumatano, Aprili 11, 2012
Nimegundua ni mume wa mtu nataka tuachane yeye anasema atanichinja akinikuta na mwanamume mwingine
Habari yako Adela mimi ni moja kati ya wadau wazuri sana wa blog yako nina shida nilikuwa na mwanamume ambaye mwanzoni wakati tunaanza mahusiano aliniambia hana mke, lakini cha ajabu nimekaa naye takribani mwaka mmoja alinifuata dada mmoja nakuniambia niachane na mume wake nilipofanya uchunguzi kweli nimegundua ni mume wa mtu baada ya kufahamu maamuzi yangu ni kuachana na huyu kaka kwani alinidanganya na mimi nilikuwa nampenda sana niliamua kuacha kupokea simu zake.
Alinifuata na kuniambia haitatokea mimi na yeye tuachane na akinikuta na mwanamume mwingine ananichinja kuna siku alinikuta nimekaa bar na marafiki zangu alianza kunipiga na kunirudisha nyumbani inaniuma anavyoyafuatilia maisha yangu huku akinipa vitisho sijui nifanyeje naombeni ushauri mimi simtaki
Jumanne, Machi 20, 2012
"Hapendi nivae kimini wakati alinitongoza nikiwa navaa nguo hizohizo ambazo sasa ananikataza nisivae"
Alhamisi, Machi 01, 2012
"Nachukia tabia ya kaka yangu kunifuatilia na kugombana na marafiki zangu wa kiume"
Habari yako Adeladally mimi naitwa Salima ni mkazi wa Dar es salaam nipo kidato cha sita tatizo langu ni kuhusu kaka yangu ana tabia ya kumfuata kila mwanamume ninayeongozana naye na kumpa onyo asiwe karibu na mimi hiki kitu kinanikera sana kwani anasababisha mimi nakosa marafiki, nilishawahi kumuambia sipendi hiyo tabia akaniambia atakuja kuwavunja miguu wanaume atakaowakuta karibu na mimi, ukweli ni kwamba huyo kaka yangu ndiye anayenilipia ada ya shule lakini sasa ananichunga hadi nakosa raha.
nilikuwa na boyfriend wangu hivi majuzi alitukuta tumekaa tunazungumza alimshika yule boyfriend wangu na kumpiga sana na hadi hivi sasa yule boyfriend wangu hataki kuonana na mimi jamani sijui nimfanyeje huyu kaka yangu yaani hataki mimi kuwa na ukaribu na wanaume inaniboa sana.
nilikuwa na boyfriend wangu hivi majuzi alitukuta tumekaa tunazungumza alimshika yule boyfriend wangu na kumpiga sana na hadi hivi sasa yule boyfriend wangu hataki kuonana na mimi jamani sijui nimfanyeje huyu kaka yangu yaani hataki mimi kuwa na ukaribu na wanaume inaniboa sana.
Jumatano, Februari 15, 2012
"sikukuu ya Valentine nilitegemea ningekuwa na mwenza wangu cha ajabu simu yake ilikuwa haipatikani leo ananipigia ananiambia alipata dharura "
Jamani mimi ni mwanamke naombeni ushauri huyu mwanamume nahisi ananidanganya siku ya valentine aliniahidi tungekuwa pamoja, cha ajabu simu yake ilikuwa haipatikani nilihuzunika sana sasa leo ananipigia simu anasema alipata dharura alikuwa nje ya mji, ukweli mimi iliniuma na kuamua kwenda nyumbani kwake kwani funguo ya nyumbani kwake ninayo nilichokikuta ni zawadi zimetoka kwa mwanamke ikiwemo kadi na vitu vingine aliporudi na kunikuta nimeingia naangalia hivyo vitu amekuwa mkali na kusema ni vya rafiki yake.
Nilimuuliza, kama ni vya rafiki yake vinafanya nini hapo? akanijibu rafiki yake alishinda hapo sikumuamini nikamwambia anipe namba ya huyo rafiki yake nimpigie kumuuliza alikasirika na kusema eti nataka kumuaibisha kwa rafiki zake kuwa mimi simuamini na namuona yeye malaya yaani roho inaniuma sana kwa jinsi ninavyompenda sijui nifanyeje
Nilimuuliza, kama ni vya rafiki yake vinafanya nini hapo? akanijibu rafiki yake alishinda hapo sikumuamini nikamwambia anipe namba ya huyo rafiki yake nimpigie kumuuliza alikasirika na kusema eti nataka kumuaibisha kwa rafiki zake kuwa mimi simuamini na namuona yeye malaya yaani roho inaniuma sana kwa jinsi ninavyompenda sijui nifanyeje
Jumapili, Februari 12, 2012
"Kutokana na aliyonifanyia inaniuma sana nimemsamehe lakini nashindwa kuwa na upendo kama ilivyokuwa mwanzo naombeni ushauri nifanyeje"
Mambo dada ade, mimi ni msichana nilikuwa naomba ushauri. nina rafiki yangu ambaye anatoka africa magahribi ninasoma nae nje ya nchi. tuko chuo tunamaliza mwaka wetu wa mwsho. huyu binti ana tabia ya kutokukaa na marafiki kwa muda mrefu kwa sababu ana attitude problem lakini kwa mimi imekuwa tofauti tumeweza kuwa friends tangu 2009.
kulikuwa na visa vingi lakini mimi ni mtu ambaye naweza kuishi na mtu yeyote hata awe na tabia zipi so she respects the fact that i take her shit . ok jambo lenyewe ni hili, huyo rafiki yangu ana boyfriend wake ambaye aliwahi kunitongoza na nikamtolea nje. baada ya hapo akaanza kunichukia sana na kumwambia rafiki yangu asiwe karibu na mimi.
Kabla ya hilo jambo tulikuwa karibu sana na walikuwa wanapenda sana company yangu so hata tulivyokuwa tukitoka ama weekend nilikuwa naspend kwao. na tulikuwa tunalala kitanda kimoja. . basi baada ya kumtolea nje aliweka kinyongo. weekend moja tulitoka na tuliporudi wakasema kwamba its late ku drive kunirudisha kwangu kwa hiyo nitalala kwao asubuhi watanirudisha.
Basi nikalala na baada ya muda kidogo yule rafiki yangu akaenda chooni, akiwa chooni huku nyuma yule boyfriend wake akaanza kunishika makalio nikatoka kitandani na kumkimbia na baadaye yule rafiki yangu akarudi . nilipoamka asubuhi wakanirudisha kwangu. kumbe yule mwanaume alipanga kunifanyia kitu kibaya kupitia rafiki yake. alimpa namba anitongoze alale na mimi na anifanyie kitu kibaya .
Mimi nikawa nimekasarikia kwa nini ampe namba yule mtu anitake kimapenzi, nikaamua kumuuliza kwanini alimpa namba yule rafiki yake mimi sio malaya.. basi akakasirika eti kwanini nimemuuliza akamwambia rafiki yangu mambo mengi ya uongo kuhusu hiyo ishu wakati mimi nilimuuliza tu wala sikumtukana . basi wakanishambulia wakanitukana ilikuwa siku ya mwaka mpya.
Nililia sana na niliumia na baadaye yule msichana akaja kuniomba msamaha nimesamehe lakini nimetokea kumchukia ingawa namchekea tu usoni.. naomba ushauri manake naona moyo unakuwa mzito kuwa na upendo niliokuwa nao mwanzo,..
Jumatatu, Januari 30, 2012
"Simpendi mwanamume anayetaka kunioa nahisi nitaolewa kwa kuogopa laana ya wazazi"
Mimi ni mwanamke naishi na wazazi wangu ambao nawapenda sana wamenilea na kunipa kila ninachokitaka nimesoma na kwa sasa nafanya kazi tatizo linakuja hivi karibuni wazazi wangu walinitambulisha kwa mwanamume ambaye wanataka mimi niolewe naye ukweli ni kwamba mimi huyo mwanamume sijampenda na pia anaumri mkubwa kuliko hata mimi yaani anaweza hata kuwa baba yangu,, ila baba na mama wananiambia nisingesoma hadi hapa nilipo bila ya huyu mwanamume kwani amekuwa akiwasaidia wazazi wangu kwa kiasi kikubwa na alinipenda mimi tokea nikiwa mtoto mdogo,, binafsi mimi ninaye mchumba ambaye nimemueleza hali halisi alichoniambia mchumba wangu nitoroke nyumbani nikaishi mbali yeye atanisaidia,, lakini nikifikiria mimi ni mtoto wa pekee kwa wazazi wangu nilikuwa na kaka na mdogo walishafariki zamani kidogo,, na pia wazazi wangu wananiambia nisipoolewa na huyo mwanamume waliyenichagulia wataniachia laana hapa nilipo nakosa raha kila nikifikiria kuanza maisha na mtu nisiyempenda naombeni ushauri wenu
Jumatano, Januari 04, 2012
Naitwa Zuhura" Jamani huyu mwanamume ananiaibisha mambo yetu ya chumbani anawasimulia marafiki zake"
Mambo vipi Adela mimi ni mfuatilia sana wa Blog yako naomba uniwekee ujumbe huu nipate ushauri, jamani mimi ninaye mchumba nampenda sana na tumekuwa katika mahusiano takribani mwaka mmoja na nusu lakini tatizo mwenzangu sijui anatabia gani kwani mambo yangu yote anayoyajua anawaambia marafiki zake kuna kipindi niliwahi kumuambia kuhusu tabia yake lakini imekuwa vigumu kubadilika kwani hivi majuzi nilikutana na rafiki yake mmoja maneno aliyoniambia kiukweli nilishangaa eti aliniambia "shemeji mambo yako makubwa anatuambia tu bwana ako kwamba umekamilika kila idara yaani akanitajia hadi nguo ya ndani nayopenda kuvaa na mambo mengine ya aibu yaani nilihisi kama nimevuliwa nguo hii tabia inanikera sana yaani marafiki zake wengine wanadiriki kuniambia shemeji wewe kwa viduku kitandani tunasikia unaweza sana sasa jamani huyu mwanamume nimfanyeje kwasababu yamenifika kooni natamani hata kumuaibisha inaniuma sana sikutegemea kama yupo hivyo.
Jumatano, Novemba 23, 2011
"zamani tulikuwa tunabusiana na kukumbatiana mara kwa mara, pia aliniita majina kama honey,,baby, darling lakini siku hizi hakuna tena"
MAPENZI MATAMU NI YALIYOJAA UAMINIFU, FURAHA, UPENDO NA AMANI UKIMYA HAUJENGI BALI UNABOMOA.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





