Jumatano, Novemba 06, 2013

Dada Lusi anaomba ushauri "Nimeishi na mume wangu muda mrefu lakini namuogopa sana sijui nifanyeje"

Habari yako dada Adela naomba uisaidie kuweka kwenye blog yako mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36, nimeolewa nina watoto wawili, tatizo ni kwamba namuogopa sana mume wangu, yaani tokea nilipoolewa nimekuwa nikimuheshimu na kumsikiliza kwa kila jambo. Tatizo linakuja hata akinikera nashindwa kumueleza ukweli nabaki nalo moyoni bila ya kumuambia nini kinanisumbua.

 hali hii pia inanifanya nashindwa kuwa muwazi katika mapenzi yetu kwani hata kama hajaniridhisha basi huwa namwambia nimeridhika. Naichukia sana hii hali lakini sijui nifanyeje. Yaani nikimuona tu nakuwa na hofu na aibu pia, natamani kubadilika naombeni ushauri jamani. Kwani najikuta nashindwa hata kuzungumza naye mambo ya msingi katika maisha yetu. 

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom