ILIPOISHIA“Jamani za siku nyingi.” Aliendelea kumsemesha
Julieth. Mwanzo Julieth hakumtambua lakini alivyozidi kumwangalia akamkumbuka.
“Oh! Kumbe Zubeda! Mambo vipi rafiki yangu?
Nimefurahi sana kukuona habari za hapa?” Zubeda alikuwa ni rafiki yake Julieth,
kwani walikuwa wakiuza chapati pamoja wakati Julieth akiwa Arusha. Domina alianza kulia, haraka Zubeda alimchukua
Dominiki ili Julieth amnyonyeshe Domina. USIKOSE SURA YA 11
INAPOENDELEA
“Habari za hapa ni nzuri kiasi.” Aliongea Zubeda huku
akimshika vizuri mtoto.
“Nzuri kiasi!” Alihamaki Julieth huku akimkazia macho
Zubeda.
“Ndiyo! Nzuri kidogo.” Alisisitiza Zubeda huku
akiyakwepa macho ya Julieth.
“Vipi mwenzangu
mbona ulikuwa kimya sana? Wakati mama yako akiwa anaumwa tulikupigia simu mara
nyingi lakini haikupatikana na …”
“Ehe! Sasa anaendeleaje?” Julieth alimkatisha Zubeda
na kuuliza akiwa katika hali ya kushtuka.
Zubeda
aliwachukua watoto wa Julieth na kukaa nao pembeni wakati yule dereva
akiondoka. Julieth alitaka kuingia ndani moja kwa moja lakini Zubeda alimzuia.
“Julieth
wadogo zako na mama yako hawapo hapa.” Zubeda alianza kueleza.
Kama nilivyokudokeza mama yako aliugua sana,
tulikutafuta kwenye simu yako ili utume fedha za matibabu bila mafanikio. Kwa
vile mama yako alikuwa hana pesa ikabidi auze simu yake ili apate pesa za
matibabu.”
“Oh! Samahani sana. Simu yangu iliharibika nikawa na
simu nyingine. Lakini namba ya mama ninayo, ila nilishawahi kumpigia lakini
haikupatika. Labda ndo kipindi
alipoiuza. Aliongea Julieth kwa masikitiko.”










