Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo JE WEWE UNASEMAJE. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo JE WEWE UNASEMAJE. Onyesha machapisho yote

Jumatano, Juni 12, 2013

INASEMEKANA WANAUME WALIO WENGI HAWAPENDI KUTUMIA KINGA WAKATI WA TENDO.

Imefahamika  kuwa Baadhi ya wanaume walioathirika na virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ni wagumu kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa na kusababisha maambukizi mapya katika familia zao.

  Hayo yamesemwa Mwanamke mmoja ambaye hakutaka kuweka jina lake bayana alisema, kutokana na tabia hiyo, wanawake hujikuta wakilazimika kufanya tendo la ndoa ambalo si salama hali inayochangia ongezeko la maambukizi mapya.

Na jambo hili si kwa waathirika pekee bali watu wote ni vyema kutumia kinga  au kupima afya yako na mwenzako mara kwa mara kumbuka UKIMWI UPO NA HAUNA DAWA.Kuna kauli moja hupendwa kutumiwa na baadhi ya watu kuwa "siwezi kula pipi na maganda yake" Haya ni maneno yananayopotosha. KUWA SALAMA KWA KUTUMIA KINGA.

Jumatatu, Aprili 29, 2013

"HATAKI NIIJUE PASSWORD YAKE ANAYOTUMIA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KAMA FACEBOOK NA TWITTER NAHISI ANANISALITI"

Je unafikiri kuna umuhimu wa kuifahamu password ya mwenza wako anayotumia katika mitandao ya kijamii?? Kuna dada mmoja alinitumia ujumbe na kuniambia kuwa anahisi mpenzi wake anamsaliti kwasababu hataki kumpa neno lasiri analotumia kuingia kwenye facebook page yake pamoja na twitter.

Inawezekana kuna baadhi ya wapenzi ambao hufanya hivyo kwamba kila mmoja anajua password anayotumia mwenzake na yupo huru kufungua na kufanya chochote. Lakini pia wapo ambao hawataki hata wenza wao wajue kama wamejiunga kwenye mitandao ya kijamii. Katika hili ni makubaliano  baina ya wawili wapendanao lakini jamani kama kweli mnapendana na uaminifu kwenu upo kwa asilimia zote haina haja ya kufichana password ni kuwa huru tu na kujiamini. JE WEWE UNASEMAJE



Jumanne, Desemba 11, 2012

WIVU WA MAPENZI KIKWAZO CHA MAENDELEO

Wiki iliyopita huko mkoani Tanga  kulikuwa na mjadala wa mdahalo wa usawa wa kijinsia ulioandaliwa  na Muungano wa Asasi za Kiraia Wilaya  ya Lushoto , katika  mdahalo huo Wivu umeelezwa kuwa kikwazo cha maendeleo ndani ya jamii kutokana na wanaume kuwazuia wake zao kuwajibika katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali wakihofu kusalitiwa jambo lililodaiwa kuongeza umasikini katika familia .

. Inawezekana kuna sababu za kimila na kadhalika ambazo zinamfanya mwanaume  asimpe nafasi mke wake katika  kushiriki kwenye shughuli mbalimbali kwaajili ya kujipatia kipato lakini hili suala la wivu mnalionaje jamani kwamba mwanaume anahisi mwanamke akiwa kazini atakuwa na wanaume wengine mimi sidhani kama ni jambo la busara kwani mtu kama anaamua  kuanzisha mahusiano hata kama akiwa hana kazi  anaweza  kufanya usaliti JE WEWE UNASEMAJE

Jumatano, Oktoba 17, 2012

Je ni sahihi mwanamke kumsachi mwenza wake ili kujua kiasi cha pesa aliyonayo.

kuna baadhi ya wanawake wanayotabia ya kuwasachi wenza wao pale ambapo akimuomba hela  akiambiwa sina pesa basi anaanza kumsachi ili kuangalia kama kweli anayo pesa au la, au wakati mwingine hata kabla ya salamu moja kwa moja unakimbilia kwenye mfuko wa shati au wa suruali na kutaka kujua kiasi cha pesa aliyonayo,Baadhi ya wanaume wameilalamikia tabia hiyo kutokana na namna mwanamke anavyompekuwa na kutaka kujua ana pesa kiasi gani, hususani ambao hawajafunga ndoa JE WEWE UNASEMAJE KWA WALIO KWENYE NDOA INAWEZA KUWA NI POA  AU NI KERO..........

Jumatano, Julai 11, 2012

duuuh

Hapa ni wodi ya kinamama wajawazito  embu tizama walivyojazana na wengine kulala chini UBORESHWAJI UNAHITAJIKA JAMANI

Jumanne, Juni 12, 2012

Alama za FREEMASON ZAENDELEA KUTAPAKAA

Jamaa aliniambia hii ni swaga tu
Nikafananisha na hii hivi kuna ukweli kuhusu hizi alama jamani mi nahisi labda ni swaga tu kwasababu wengine hutumia bila hata kujua maana yake kwasababu sikuhizi kila unachokifanya utasikia kinahusishwa na jambo fulani

Vijana walikuwa wanasalimiana kama hivi


Alhamisi, Juni 07, 2012

Je hili nalo lina ukweli wewe unasemaje,,,ameandika Joel Ngerema kutoka facebook

Wanawake karibu 98% wanataka hivi vigezo....NICE CAR,NICE HOUSE NA ATM CARD IWE INAONGEA asa jamani maskini wenzangu tunafanyaje? si wenye  hizo qualifications wataendelea kutamba na kuringa?.....dunia haiko fea kwa kweli

Jumanne, Juni 05, 2012

Nguo hizi zinachochea vishawishi

Mtazame babu anavyomkodolea macho mdada aliyevalia skintyt  inawezekana kwa kiasi kikubwa baadhi ya mavazi ya kina dada kuchochea vishawishi jambo la msingi ni kuvaa mavazi kulingana na sehemu unayokwenda kwasababu usipokuwa makini unaweza kujikuta unajiaibisha

Jumatano, Mei 23, 2012

Swali kutoka kwa Dayna facebook,,Je wewe unasemaje

X'' wako mlisitisha uhusiano then akaoa ama kuolewa'' na kila mmoja akaridhika na hilo,, baada ya ndoa anaibuka nakuta mrejeshe uhusiano kwamba ameshindwa kuvumilia kuwa mbali na ww na siku zote amekosa amani na kujutia kwa uamzi aliofanya wa kuoa ama kuolewa'' kwani hajui hata kwanini alioa alijukuta anafanya hivo ghafla,,anakosa raha, usingizi,ari ya kazi,, yuko tayari kwa mapenzi ya dhati'' kibaya zaidi anakuonea wivu sana kwa mpenzi mpya ulienae,, ungekuwa ww ungefanyaje?

Baadhi Wanawake wanaongoza kulia shida kama kuomba pesa mara kwa mara

Ni kweli hii tabia ipo kwa baadhi ya wanawake katika mahusiano yaani yeye muda wote anachokiwaza ni hela kila anapokutana na  mwenza wake anawaza atamuachia pesa kiasi gani akimpigia simu anaomba hela,, je inamaana hii ni tabia au  ukiwa na mpenzi ni lazima kila tatizo ulilonalo akusaidie???? ndiyo maana kauli hii ya MAPENZI YA SIKU HIZI NI HELA inatawala sana

Jumatano, Mei 16, 2012

Katika hili unajikuta katika wakati mgumu sana

Picha hii nimeikuta Facebook ukweli mambo hayo yakikukuta inahitaji moyo hapo ndipo wengine wanakata tamaa ya maisha lakini ni vyema kupiga moyo konde na kufanya kazi kwa bidii

Jumapili, Mei 06, 2012

Nimeyapenda sana haya maneno

Binadamu tunakutana na changamoto nyingi sana, katika haya maisha lazima ukubali kuna atakayependa ama kufurahia kazi yako, lakini pia kuna wale ambao wapo kwaajili ya kukosoa kazi yako yaani hata kama ufanye vizuri lazima kuna atakaye kukosoa  ama kupinga kile unachokifanya wengine husema hali hii hutokana na wivu, choyo, chuki ama wengine hukosoa wakiwa na nia  nzuri ya kuelimisha JE WEWE UNASEMAJE.

Ujumbe wangu Leo UPENDO NA FURAHA KATIKA FAMILIA YAKO UNAJENGWA NA WEWE MWENYEWE.

Kuwa karibu na familia yako mfano kila Jumamosi ama Jumapili mmezoea kujumuika pamoja nyumbani, kwa mlo wa mchana; badili mfumo huo kwa kupeleka familia yako hotelini, au ufukweni  kupata mlo wa mchana angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu. Yaani mara nne tu, kwa kila mwaka ambapo mnaweza kucheza michezo mbalimbali na kufurahia maisha kwa pamoja.

KUJENGA familia bora na yenye furaha kunahitaji uwajibikaji na kujituma kwa kiwango cha juu. Kwa ujumla, mtu anatakiwa atoe kipaumbele kwa familia.


Zipo familia ambazo, watoto wanaisahau sura ya baba yao. Kwa sababu baba hurudi usiku sana na kuondoka alfajiri. Kukaa pamoja na familia yako, kutakupa mwangaza bora wa wapi pa kurekebisha. Hudumia vyema familia yako Namna tunavyo hudumia familia zetu ni muhimu sana. 

Kila siku, kila wakati, mtazamo wa mtu unahusika katika hili.Inapotokea ‘ukaangushwa’ na mmoja wa wapendwa katika familia yako usihamaki, usimuhukumu wala kumuumiza kwa kudhamiria badala yake muepuke au ondoka kwa wakati huo. Daima onyesha upendo, jiweke kuwa muhimili wa wanafamilia yako na hata kama mkitofautiana, hakikisha unabaki mkarimu kwao.

Hata kama mmefanikiwa kujenga familia yenye furaha, wewe au mmoja wa wapendwa wako hamuwezi kukwepa huzuni, mambo yanayogusa mioyo au kukwazwa katika maisha ya kila siku. Huo ni wakati mzuri kwa wanafamilia kuonyesha kuwa kila mmoja anamjali mwenzake katika kila hali; furaha na huzuni.

Jumanne, Mei 01, 2012

JE NA HILI LINA UKWELI

Nimesoma haya maneno kwa umakini kwamba kwa asilimia kubwa wanawake wazuri yaani warembo wa maumbile,sura y amekamilika kila idara siku zote ni waongo katika mapenzi na kauli hii hupenda kuizungumza baadhi ya wanaume kwamba wanawake wazuri ukiwa naye nikujipa presha Binafsi nasema inategemea na tabia ya mtu kuna walio wazuri na wametulia. JE WEWE UNASEMAJE


"Je ni kweli tabia za wanaume wote zinafanana????

Kutokana na matatizo yanayojitokeza katika mahusiano baadhi ya wanawake wamekuwa na kauli hii "yaani wanaume wote tabia zao ni moja sema tu majina ndiyo yanatofautiana" Inamaana wanaume wanaongoza kwa usaliti katika mapenzi kuliko wanawake binafsi naamini kwamba siyo wanaume wote ambao siyo waaminifu na siyo wanawake wote ambao ni waaminifu katika mapenzi JE WEWE UNASEMAJE

Jumamosi, Aprili 28, 2012

JAMANI NIMEGUSWA SANA NA MATATIZO YA SAJUKI NA WASTARA TUMSAIDIE SAJUKI,, KUTOA NI MOYO

Kutoka katika blog ya Dina nimekuwa nikifuatilia matatizo ya Wastara na Sajuki kiukweli kwa yeyote aliye na moyo wa huruma ataguswa na hili Juzi jumatano Dina alirusha mahojiano aliyoyafanya na Wastara kuhusu ugonjwa wa msanii Sajuki ambaye ni mumewe.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni toka mwaka jana mwezi wa saba.Kupitia leo tena ya clouds fm wengi mlisikia na mkaguswa kuwa sehemu ya wale wanaochangia kumwezesha Sajuki kupata matibabu nchini India mwezi ujao.


Binadamu ni vyema  kusaidiana jamani ukifuatilia mkasa mzima wa maisha ya Sajuki na Wastara yanasikitisha sana wamekutana na matukio mengi ya kusikitisha kama utakumbuka Wastara alipopata ajali na kukatwa mguu lakini Sajuki kutokana na mapenzi ya dhati aliamua kuwa naye bega kwa bega na waliishi kwa furaha na upendo huku wakiendelea na kazi zao za uandaaji wa filamu. Kwa sasa Sajuki ni mgonjwa na Wastara anaangaika huku na kule kumuombea msaada jamani kutoa ni moyo kwa chochote kidogo tumsaidie ndugu yetu NAUNGANA NA WOTE WALIO NA NIA YA KUMSAIDIA SAJUKI

Bado unaweza kuchangia kwa Mpesa 0762189592 na kupitia Akiba commercial bank acount no 050000003047 Wastara Juma.
Ingia katika Blog ya http://www.dinamarios.blogspot.com pamoja na http://www.8020fashion.blogspot.com 
kwa maelekezo zaidi nasisitiza KUTOA NI MOYO JAMANI

Ijumaa, Aprili 20, 2012

Unaweza kuitambua hali ya maisha ya mtu kwa kumtizama


Mtoto huyu anatoka katika familia duni inawezekana anawaza hata chakula hajala

Mtoto huyu hana mawazo anakula vizuri katoka katika familia bora

Tuishi kwa kusaidiana kwa aliyenacho amsaidie na yule asiyenacho

Jumatano, Aprili 18, 2012

Inawezekana kutokea haya unapodai chako,,,,,,,,,

Wakati akiwa na shida anakuja kwako huku akikuomba kwa upole na ahadi nyingi kwamba nitakurudishia siku fulani, Sasa kazi inakuja siku ya kulipa deni ataanza kukukimbia huku na kule mara simu yake ya mkononi kazima haipatikani, unamtumia ujumbe kwenye simu hakujibu,  anakuambia bado sijapata nitakulipa kesho mwisho wa siku anaanza kukununia na hata mkafikia hatua ya kuwa maadui kisa unadai chako.JAMANI DAWA YA DENI NI KULIPA.

Haipendezi kwenda na watoto kwenye ukumbi wa starehe kama club nk..

Embu muangalie huyu mtoto sasa hapo anajifunza nini? na katika hili unadhani nani wa kulaumiwa?

Alhamisi, Aprili 05, 2012

Hivi Shetani anaweza kumsababisha Baba kumbaka bintiye??

Tukio hilo limetokea Huko wilayani Maswa, Mkazi wa kijiji cha Bukangilija Tarafa ya Sengerema, Nkwambi Maganiko (38) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kufanya mapenzi na binti yake mwenye umri wa miaka 15

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Maswa Thomson Mtani baada ya ushahidi uliotolewa na mashaidi wanne wa upande wa mashtaka kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa alimbaka mwanawe huyo.Kabla ya kutoa hukumu  alisema kitendo alichokifanya  mshtakiwa huyo licha ya kuwa ni kinyume  na utamaduni wa taifa la Tanzania, pia hakikubaliki hata kidogo katika jamii na kinyume kabisa cha sheria ya makosa ya kujamiana.

Awali mwendesha mashtaka Inspekta Msaidizi wa Polisi Nurdin Ramadhani alidai kuwa Februari 2 mwaka huu majira ya saa 7:00 usiku nyumbani kwake, mshtakiwa huyo alimuamusha kutoka usingizini mke wake na kumwambia kuwa wamekuwa wachawi na hivyo watoe nguo zao zote na watoke nje.

Alidai baadaye mshtakiwa huyo aligonga mlango wa chumba cha watoto wake watatu ambao ni wasichana na kuwaamuru watoke nje wakiwa uchi na kuelekea katika mto uliokuwa karibu na nyumba yao, wakiwa njiani alimvamia mtoto wake wake huyo mbele ya watoto wake wengine na kumbaka, kitendo ambacho kilisababisha apige yowe kuomba msaada.

Kwa upande wake mshatakiwa huyo, aliiomba mahakama hiyo imwachie huru kwa madai kuwa hakufanya kitendo hicho, lakini ombi hilo lilitupiliwa mbali na kuhukumiwa kifungo hicho jela.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom