Jumapili, Mei 06, 2012

Ujumbe wangu Leo UPENDO NA FURAHA KATIKA FAMILIA YAKO UNAJENGWA NA WEWE MWENYEWE.

Kuwa karibu na familia yako mfano kila Jumamosi ama Jumapili mmezoea kujumuika pamoja nyumbani, kwa mlo wa mchana; badili mfumo huo kwa kupeleka familia yako hotelini, au ufukweni  kupata mlo wa mchana angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu. Yaani mara nne tu, kwa kila mwaka ambapo mnaweza kucheza michezo mbalimbali na kufurahia maisha kwa pamoja.

KUJENGA familia bora na yenye furaha kunahitaji uwajibikaji na kujituma kwa kiwango cha juu. Kwa ujumla, mtu anatakiwa atoe kipaumbele kwa familia.


Zipo familia ambazo, watoto wanaisahau sura ya baba yao. Kwa sababu baba hurudi usiku sana na kuondoka alfajiri. Kukaa pamoja na familia yako, kutakupa mwangaza bora wa wapi pa kurekebisha. Hudumia vyema familia yako Namna tunavyo hudumia familia zetu ni muhimu sana. 

Kila siku, kila wakati, mtazamo wa mtu unahusika katika hili.Inapotokea ‘ukaangushwa’ na mmoja wa wapendwa katika familia yako usihamaki, usimuhukumu wala kumuumiza kwa kudhamiria badala yake muepuke au ondoka kwa wakati huo. Daima onyesha upendo, jiweke kuwa muhimili wa wanafamilia yako na hata kama mkitofautiana, hakikisha unabaki mkarimu kwao.

Hata kama mmefanikiwa kujenga familia yenye furaha, wewe au mmoja wa wapendwa wako hamuwezi kukwepa huzuni, mambo yanayogusa mioyo au kukwazwa katika maisha ya kila siku. Huo ni wakati mzuri kwa wanafamilia kuonyesha kuwa kila mmoja anamjali mwenzake katika kila hali; furaha na huzuni.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom