Jumatano, Juni 12, 2013

INASEMEKANA WANAUME WALIO WENGI HAWAPENDI KUTUMIA KINGA WAKATI WA TENDO.

Imefahamika  kuwa Baadhi ya wanaume walioathirika na virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ni wagumu kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa na kusababisha maambukizi mapya katika familia zao.

  Hayo yamesemwa Mwanamke mmoja ambaye hakutaka kuweka jina lake bayana alisema, kutokana na tabia hiyo, wanawake hujikuta wakilazimika kufanya tendo la ndoa ambalo si salama hali inayochangia ongezeko la maambukizi mapya.

Na jambo hili si kwa waathirika pekee bali watu wote ni vyema kutumia kinga  au kupima afya yako na mwenzako mara kwa mara kumbuka UKIMWI UPO NA HAUNA DAWA.Kuna kauli moja hupendwa kutumiwa na baadhi ya watu kuwa "siwezi kula pipi na maganda yake" Haya ni maneno yananayopotosha. KUWA SALAMA KWA KUTUMIA KINGA.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

MIE MTAZAMO WANGU WA KWANZA TUWE WAAMINIFU NDO NJIA PEKEE YA KUTUOKOA MAISHA YETU NA VIZAZI VIJAVYO

MIE NA MWAKA WA 10 EUROPE UKIMWI UMEANZA MIAKA MINGI NA UPO DUNIA NZIMA .

LAKINI UKIANGALIA NCHI ZA EUROPE UKIMWI SIO UGONJWA WA WENGI
WATU WAKO
WAAMINIFU
WANAISHI NA UKIMWI WAKIWA WAWAZIHATAKI KUMWAMBUKIZA MWENZAKE
HAWADANGANYI
KAMA ANAUKIMWI ANAKWAMBIA
NA MPAKA LEO DAWA HAKUNA

NCHI ZA KIAFRIKA AU ZA KIMASIKINI
MTU HAKUBALI AUMWE PEKE YAKE EMBU TUJIULIZE INASAIDIA NINI MTESEKE WENGI ????
KWANINI UMWAMBUKIZE MWENZAKO
KWANINI TUSIWE WAAMINIFU
KWANINI TUSITUMIE KINGA

TUURUMIE WATOTO WETU WANAKUJA KULELEWA NA WATU BAKI KISA TUMEAMBUKIZANA
UKIWA NA HURUMA HATA MUNGU ATAKUURUNIA


mdau uk alisema ...

HATA MIE HILI LINANICHOSHA.WAAFRICA HATUSIKIAGI SIJUI KWANINI!!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom