Jumatano, Juni 12, 2013

MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRICA KUFANYIKA SIKU YA JUMAPILI

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Africa.

Katika tamasha la mwaka huu ambalo ni la nane, ni vyema taasisi mbalimbali kujumuika pamoja na watoto kwa kula nao chakula cha mchana pamoja na kutoa zawadi  kwa watoto.

Pia ni siku ambayo watoto huonyesha vipaji vyao kama maonyesho ya maigizo,dansi, sarakasi,mavazi ya kiafrika, kwaya na kuimba mashairi.
Maadhimisho haya yanaenda sambamba na kuwatazama watoto wanaoishi katika mazingira magumu, pia kuna watoto yatima, walemavu wa viungo,wasioona,viziwi,albino. Kituo cha Sanaa Elimu na Utamaduni na Maendeleo ya Mtoto wa Africa kitaadhimisha Maadhimisho ya siku ya Mtoto Africa  kwa kula chakula cha mchana na watoto waliolazwa katika hospitali ya  Taifa Muhimbili. Ikiwa ni pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali kwa lengo la kuwafariji.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom