Tanzania
kupitia Mpango wa Damu Salama Tanzania itaungana na nchi nyengine
Duniani katika sherehe za Kuwashukuru na kuwatambua Wachangia Damu
Duniani siku ya Ijumaa ya tarehe 14 Juni, 2013 ambapo kitaifa sherehe
hizo zitafanyika katika viwanja vya Mkendo Wialyani Musoma, mkoani Mara
huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mwenye dhamana Katika Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dk. Hussein Mwinyi.
Kwa
Mujibu wa Mpango wa Damu Salama Tanzania, wananchi ambao wako katika
mikoa mengine nje ya kanda ya ziwa wanaweza kujumuika na vituo vya Damu
Salama vilivyo katika kanda zao ili kuweza kusheherekea na kujitolea
damu siku hiyo.
Aidha,
sehemu zilizoanishwa na Mpango wa Damu Salama Tanzania ambapo sherehe
hizo zitafanyika Kimkoa ni Makao Makuu ya Mpango wa Damu Salama
Tanzania, Ilala Mchikichini kwa Mkoa wa Dar es salaam, Viwanja vya
Tangamano kwa Mkoa wa Tanga, Mkoani Tabora Katika Kituo cha Damu Salama
Kitete, Viwanja vya Luanda Nzovwe Jijini Mbeya, Kwa wilaya ya Kilwa
mkoani Lindi sherehe zitafanyika katika Bustani ya Mkapa, Morogoro
katika Kituo cha Damu Salama Rwegosore, na Mkoani Lindi katika kituo cha
Damu Salama Ilulu.
Sherehe
hizo za Kila mwaka zinalengo la kuamsha ari pamoja na kuongeza uwelewa
juu ya mahitaji ya damu na umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili
kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu duniani ikiwa pamoja na
kuwashukuru na kuwapongeza wachangia damu wote duniani.
Kidunia sherehe hizi zitafanyika Jijini Paris, Ufaransa chini ya
Shirika la Afya Duniani (WHO) ikishirikiana na Shirikisho la Kimataifa
la Msalaba Mwekundu (IFRC), Shirikisho la Kimataifa laTaasisi za
Kuchangia Damu (IFBDO), na Jumuiya ya Kimataifa Mpango wa Damu Salama
(ISBT). Ujumbe wa Mwaka huu ni TOA ZAWADI YA MAISHA. CHANGIA DAMU.
Rafiki
wa Damu Salama Tanzania inawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi
siku ya Ijumaa kuweza kujumuika pamoja katika sherehe hizi muhimu ambazo
zinagusa moja kwa moja maisha ya mwanadamu. Mahitaji ya damu nchini
bado ni makubwa na wahitaji wamekuwa wakiongezeka kila siku kutokana na
Uzazi kwa kina mama, ajali na magonjwa ya saratani. Kama asilimia 1% tu
ya watanzania watajitolea kutoa damu kwa mwaka basi Tanzania itaweza
kuondokana na tatizo hili la upungufu wa damu.
|
Maoni 1 :
Tupo pamoja
Chapisha Maoni