Jumanne, Desemba 11, 2012

WIVU WA MAPENZI KIKWAZO CHA MAENDELEO

Wiki iliyopita huko mkoani Tanga  kulikuwa na mjadala wa mdahalo wa usawa wa kijinsia ulioandaliwa  na Muungano wa Asasi za Kiraia Wilaya  ya Lushoto , katika  mdahalo huo Wivu umeelezwa kuwa kikwazo cha maendeleo ndani ya jamii kutokana na wanaume kuwazuia wake zao kuwajibika katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali wakihofu kusalitiwa jambo lililodaiwa kuongeza umasikini katika familia .

. Inawezekana kuna sababu za kimila na kadhalika ambazo zinamfanya mwanaume  asimpe nafasi mke wake katika  kushiriki kwenye shughuli mbalimbali kwaajili ya kujipatia kipato lakini hili suala la wivu mnalionaje jamani kwamba mwanaume anahisi mwanamke akiwa kazini atakuwa na wanaume wengine mimi sidhani kama ni jambo la busara kwani mtu kama anaamua  kuanzisha mahusiano hata kama akiwa hana kazi  anaweza  kufanya usaliti JE WEWE UNASEMAJE

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Nakubaliana na ww kabisa ila sio kwa wanaume tu hata wanawake nao wakizidisha wivu hakutokuwa na maendeleo ndani ya nyumba.

Bila jina alisema ...

Dhana potofu hiyo ipo kwa mbali sana siku hizi kutokana na mila desturi za mahali pengine.Kuna watu bado hawajaelimika hadi leo hata ambao ni wasomi.Pia wakati mwingine ni ile hali ya sisi wanaume kudhani mwanamke akichakarika na akawa mtafutaji mzuri atakuringia au atakuwa anakuzidi maarifa na kuonekana mwanamke si kitu.Hiyo nimeiona kwa wengi hawataki kuwapa nafasi wake zao kielimu na hata kibiashara kwa kuogopa mwanamke atamkimbia akitajirika,ingawa ukweli upo maana nina ushahidi kabisa jamaa fulani wa kwetu wamekimbiwa na wake zao kwa sababu wamefanikiwa sana kibiashara na wakaungana wana wafanya biashara wakubwa na kusahau waume zao na ndoa kufa kabisa.Ni wanawake wachache pia ambao hata asome sana na afanikiwe sana wanabaki na heshima na utu kwa waume zao, wengi hubadilika sana na kujikuta wamepanda ngazi za kujenga mahusiano na wenye kiwango chao maana dili anazofanya zinafanywa na hao watu ambao lazima pawepo mikataba ya kimapenzi.Hata hivyo miaka hii nimeona wanawake wakijishughulisha sana na biashara,nikisafiri kikazi mara nyingi nakutana na wanawake humo kwenye nyumba za kulala wao ndio wadau wengi zaidi kusafirisha bidhaa kutoka huku na huko wako safarini kuliko wanaume.Hali hiyo pia inaweza kuwa kishawishi kikubwa kwa mwanamke kuingia mitegoni kimapenzi, has abiashara zinapokwama na kama wa kuzikwamua yupo hahahahahaaaaa la haulaaaa labda kama ni mcha Mungu.Kuna mwanamke mmoja kazini kwetu alisemaga wanawake wengi wafanya biashara wana watu wao wanaowakwamua katika mirija ya ufanisi wa kibiashara, japo si kila mtu.Juzi nilikuwa safarini kutoka marekani nikakutana na wadada ngangari pale Amsterdam wamesheheni bidhaa wanarudi dar ukiwacheck wako kijanjajanja tu, na tulipofika uwanja wa JK Dar ndipo niliona janja nyingine wakati wa kutoa mizigo yao unaambiwa huu mzigo wa mzee... anataja jina basi wale wapekuaji wanagusa na mkono kupapasa tu hao wanaenda mbele, du!! Usalama hamna,lakini lazima wanaume tukubali kwamba mwanamke ni mkombozi wa familia kama tutawapa nafasi tutajikomboa na tujiamini na kuwaamini, hizo dharura za njiani zikiwakuta bahati mbaya ndio njia ya mafanikio yenyewe si hata wanaume ndivyo hivyo tunapindisha kalamu maofisini unapeleka burunguti nyumbani mkeo hata hajiulizi umepata wapi wakati mshahara haufiki hata laki tano lakini leo unaleta gadi la milioni 20,kesho unasimamisha nyumba kama uyoga unaooota asubuhi mchana umechanua.

emuthree alisema ...

Ndoa ni mjumuiko wa mume na mke, na mnapo-oana mnakuwa kitu kimoja.

Inatakiwa muwe mnashirikiana kwa kila jambo bila kufichana. Uaminifu , ushirikiano na kujaliana, mkiyaweza hayo, sioni kwanini mshindwe kujipanga.

Kama mnajitosheleza , basi sio lazima wote muende kazini, kwasababu kuna ulezi wa watoto, na mlezi mnzuri wa watoto, ni mama, hili ni dhahiri.

Kama hali inakwaza, basi wote hangaikeni, na muangalie jinsi watoto wenu watakavyolelewa, tusiwatelekeze watoto wetu kwa wafanyaakzi wa nyumbani!

Ni hayo tu kwa leo mpendwa

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom