Jumatatu, Aprili 29, 2013

"HATAKI NIIJUE PASSWORD YAKE ANAYOTUMIA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KAMA FACEBOOK NA TWITTER NAHISI ANANISALITI"

Je unafikiri kuna umuhimu wa kuifahamu password ya mwenza wako anayotumia katika mitandao ya kijamii?? Kuna dada mmoja alinitumia ujumbe na kuniambia kuwa anahisi mpenzi wake anamsaliti kwasababu hataki kumpa neno lasiri analotumia kuingia kwenye facebook page yake pamoja na twitter.

Inawezekana kuna baadhi ya wapenzi ambao hufanya hivyo kwamba kila mmoja anajua password anayotumia mwenzake na yupo huru kufungua na kufanya chochote. Lakini pia wapo ambao hawataki hata wenza wao wajue kama wamejiunga kwenye mitandao ya kijamii. Katika hili ni makubaliano  baina ya wawili wapendanao lakini jamani kama kweli mnapendana na uaminifu kwenu upo kwa asilimia zote haina haja ya kufichana password ni kuwa huru tu na kujiamini. JE WEWE UNASEMAJE



Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Ndio maana watu wanakorofishana kienyeji hivihivi kwa kudhani kuwa kupenda kuko kwenye password. Kujua password ya mkeo/mpenzio kunakupa faida gani?kwani maisha yenu yamebebwa na mambo ya mityandaoni?Kila kukicha watu wanafikiri kusalitiwa tu du kizazi hiki balaa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom