Tukio hilo limetokea Huko wilayani Maswa, Mkazi wa kijiji cha Bukangilija Tarafa ya Sengerema, Nkwambi Maganiko (38) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kufanya mapenzi na binti yake mwenye umri wa miaka 15
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Maswa Thomson Mtani baada ya ushahidi uliotolewa na mashaidi wanne wa upande wa mashtaka kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa alimbaka mwanawe huyo.Kabla ya kutoa hukumu alisema kitendo alichokifanya mshtakiwa huyo licha ya kuwa ni kinyume na utamaduni wa taifa la Tanzania, pia hakikubaliki hata kidogo katika jamii na kinyume kabisa cha sheria ya makosa ya kujamiana.
Awali mwendesha mashtaka Inspekta Msaidizi wa Polisi Nurdin Ramadhani alidai kuwa Februari 2 mwaka huu majira ya saa 7:00 usiku nyumbani kwake, mshtakiwa huyo alimuamusha kutoka usingizini mke wake na kumwambia kuwa wamekuwa wachawi na hivyo watoe nguo zao zote na watoke nje.
Alidai baadaye mshtakiwa huyo aligonga mlango wa chumba cha watoto wake watatu ambao ni wasichana na kuwaamuru watoke nje wakiwa uchi na kuelekea katika mto uliokuwa karibu na nyumba yao, wakiwa njiani alimvamia mtoto wake wake huyo mbele ya watoto wake wengine na kumbaka, kitendo ambacho kilisababisha apige yowe kuomba msaada.
Kwa upande wake mshatakiwa huyo, aliiomba mahakama hiyo imwachie huru kwa madai kuwa hakufanya kitendo hicho, lakini ombi hilo lilitupiliwa mbali na kuhukumiwa kifungo hicho jela.
Maoni 3 :
Huko ndiko dunia inapokwenda, ukingoni...tumuombe mungu atunusuru, najua shetani atasingiziwa mengi, na hata siku ya mwisho atashangaa na kulalamika,`mbona mimi sijawahi kumshawishi mtu huyu afanye hayo, hayo hata mimi siyajui...' maana sisi wanadamu sasa hivi tunafanya hata yale ambayo shetani hayafanyi...yalivyozidi ubaya...
Mambo mengine mpaka shetani anasingiziwa! Kubaka kwingi husababishwa na nyege tu aisee!
Ni moja ya mtazamo tu!:-(
Mimi naona kama adhabu haitoshi labda ndiyo maana haya matukio yamekuwa yakijirudia mara kwa mara
Chapisha Maoni