“Pole sana mama mwili wa mumeo upo katika chumba cha …..? Kabla ya kumaliza kusema mama Julieth alianguka chini na kupoteza fahamu. Haraka wale askari walimbeba Mama Julieth na kumwingiza katika chumba maalumu ambako alipata huduma na kupata fahamu baada ya saa 3. Kisha daktari aliwaomba wale askari kumsindikiza mama Julieth nyumbani kwake.
INAPOENDELEA
Majirani
zake mama Julieth walikwisha kusanyika nyumbani huku mmoja wao
akienda shuleni kuwafuata watoto. Baada ya kufika mama Julieth vilio na kelele
za kila aina vilitawala huku mama Julieth akianguka chini nakukosa
nguvu kabisa. Mipango ya mazishi ilifanyika na kuamua kuzika siku
iliyofuata. Siku ya
mazishi watu walijaa sana huku simanzi na masikitiko vikitawala katika
eneo lote la Kaloleni kwani Mzee Magesa alikuwa maarufu sana.
Mwili wa
Mzee Magesa ulizikwa kwa taratibu zote huku viongozi wa dini na
serikali kutoka Kaloleni wakihudhuria na kutoa nasaha zao. Huo ndio ulikuwa
mwisho wa maisha ya Mzee Magesa ‘Muuza mboga’
sokoni. Wiki mbili
baada ya mazishi Mama Julieth alikuwa bado hajapata nguvu za kuanza
kufanya chochote. Siku moja alikuwa amekaa katika ngazi amejiinamia
kama mtu ambaye amekata tamaa ya maisha, akiendelea kulia kwa
uchungu. Julieth alitoka ndani akiwa ameshika kikombe cha chai na kumpa mama
yake huku akimfariji.
“Mama
usilie, sisi tupo na wewe Mungu atatusaidia.” Julieth alimfariji mama yake
huku akimpa chai. “Mwanangu
baba yenu alikuwa nguzo ya familia na sasa hayupo tena. Kumbuka
mnatakiwa msome nani atawasomesha? Hivi ni kwa nini Mungu
amemchukua mapema hivi?” Alijibu mama Julieth huku akibubujikwa
na machozi. “Mama
tusikate tamaa hata baba kabla hajafariki alisema tuwe na mshikamano
na upendo katika familia yetu. Mama mimi nitakuwa nawe bega kwa
bega kukusaidia.” Julieth aliendelea kumfariji mama yake.
Mama
Julieth alimwangalia Julieth kwa macho ya matumaini kisha akamkumbatia
mwanawe. “Sawa
mwanangu kwani yote haya ni mapenzi ya Mungu.” Alijibu mama Julieth na
kuanza kunywa chai. Basi
Julieth aliendelea na kazi za ndani na kumwacha mama yake akiwa amepumzika.
******************************************************
Baada ya
mwaka mmoja kupita tangu Mzee Magesa afariki mama Julieth aliugua
ugonjwa wa moyo, kwa hiyo akashindwa kuendelea kufanya kazi zake za
kila siku na hata biashara ya sokoni aliyokuwa akiifanya baba Julieth hakukuwa
na mtu wa kuwasaidia kuiendeleza. Hali ya kipato ilizidi kuwa ngumu
kutokana na kuugua kwa mama Julieth kwani hata kazi ya kupika
chapati hakuweza kuendelea nayo tena. Kutokana
na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu Julieth aliamua kuacha shule
akiwa Darasa la Sita ili kumsaidia mama yake kazi za pale nyumbani na ikiwa
ni pamoja na kuuza chapati.
Julieth
alianza kuuza chapati biashara ambayo haikuwapa kipato kikubwa kuweza
kujikimu kutokana na wateja kuwa wachache. Kutokana na maisha kuwa
magumu walilazimika kula mlo mmoja kwa siku ili kukusanya kodi ya vyumba
viwili walivyokuwa wanaishi. Julieth aliendelea kuvumilia bila kukata
tamaa kwani mbali na kuwa ni binti mdogo lakini alikuwa na majukumu
makubwa ya kutunza familia. Katika
kuuza chapati Julieth alikutana na watu mbalimbali waliozipenda sana
chapati alizokuwa akipika. Siku moja asubuhi alikuja kaka mmoja kununua
chapati akatokea kumpenda sana Julieth.
“Habari
yako mrembo!” Yule kijana alimsalimia Julieth huku akitabasabu. “Nzuri
kaka karibu.” Alijibu Julieth huku akimwangalia usoni. “Mimi
naitwa John sijui mwenzangu unaitwa nani?”Alijitambulisha yule kijana. Julieth
alisita kidogo halafu akajibu; “Naitwa
Julieth karibu kaka chapati shilingi mia moja na hamsini nikupe chapati
ngapi?” Alijibu Julieth. “Naomba
chapati mbili.” Alitamka John huku akimpa noti ya shilingi elfu kumi.
“Mmh
jamani huna hela ndogo kaka au kuna kitu kingine unataka kununua
dukani nikakuchukulie, asubuhi hii chenchi zinasumbua kweli.” Alisema
Julieth kwa kulalamika.
“Usijali
Julieth nipe hizo chapati na fedha inayobaki ni zawadi yako.” Alijibu
John. “Mh we
kaka, hela yote hii nibaki nayo kuna usalama kweli? Hapana kaka ngoja
nikutafutie tu chenchi.” Alisema Julieth huku akinyanyuka kwenda dukani. USIKOSE SURA YA .....4.....
Maoni 1 :
Tupo pamoja mpendwa
Chapisha Maoni