Baada ya mapenzi na raha kushamiri, Julieth alipata ujauzito ambao hakugundua kama ana mimba. Aligundua baada ya kwenda hospitali kupima afya yake kutokana na kutojisikia vizuri ikiwa ni pamoja na kusikia kichefuchefu. Suala la mimba lilimfurahisha sana Julieth. “Huu ndio wakati mwafaka wa kufunga ndoa, najua John atafurahi sana nikimzalia mtoto. Akija leo nitamwambia tufanye haraka tufunge ndoa.” Aliwaza Julieth. USIKOSE SURA YA ......7.........
INAPOENDELEA
Ilipofika
jioni aliandaa chakula cha usiku mapema huku akiwa anamsubiri mpenzi
wake arudi ampe taarifa kuhusu mimba aliyonayo. John alirudi na kumkuta
Julieth anafuraha sana. “Kulikoni
leo mpenzi mbona unaonekana una furaha sana kuna nini?” Aliuliza
John. “Mpenzi leo
nimetoka hospitali kupima nina ujauzito wako na sasa nadhani
utakuwa muda mwafaka tufanye haraka tufunge ndoa.” Aliongea Julieth
huku akitabasamu na kujichekeshachekesha.
”Ni vizuri
Julieth lakini kwanza ukisha jifungua ndio tutafunga ndoa.” Alijibu John
akionyesha kutofurahishwa na taarifa ya Julieth kuhusu ujauzito. “Jamani
John ni muda mrefu tumekuwa pamoja kwa nini isiwe mapema kabla
sijajifungua?.” Alisisitiza Julieth huku akimsogelea na kuweka mikono
yake mabegani kwa John. “Sikiliza
Julieth nikwambie; ndoa ina mipango mingi sana kwa hiyo wewe nisikilize
mimi.” Alisema John huku akiwa anainuka na kuelekea chumbani.
John
alikuwa kama mtu ambaye hajafurahia habari alizopewa na Julieth, basi
Julieth alinyamaza kimya lakini aliendelea kufikiri na kutafakari hali aliyoonyesha
John baada ya kupewa taarifa ya ujauzito. “Mbona
John amebadilika ghafla kuna nini? Ngoja nimwache nitamwambia
kesho vizuri.” Aliwaza Julieth huku akimfuata John .Kesho yake
asubuhi kama kawaida waliamka mapema sana, Julieth aliandaa
chai. Walipokuwa wanakunywa Julieth alimwambia John kuwa angependa
kwenda Arusha kuwaona mama na wadogo zake kwani ilikuwa ni muda
mrefu.
“John
naomba niende Arusha nikamsalimie mama na wadogo zangu.” Aliomba
Julieth.
“Huko
Arusha tutakwenda wote siku nitakayopanga mimi, tena nikipata muda.”
Alijibu John akiwa amenuna. “Vipi John
mbona umebadilika tangu jana naona haupo sawa tukiwa tunazungumza
unaonekana una hasira kuna tatizo gani?” Julieth alihoji. “Tatizo ni
wewe unaongea sana sipati hata muda wa kupumua, tena na hii chai
kunywa mwenyewe.” Akaondoka na kumwacha Julieth akiwa ameduwaa. “Huyu
mwanamume amekuwaje mbona hivi jamani simuelewi.” Aliwaza Julieth.
Basi
Julieth akaondoa vyombo mezani na kuendelea na shughuli zake. Kadiri
siku zilivyozidi kusonga mbele tabia ya John ilizidi kubadilika. Alianza
kuchelewa kurudi nyumbani na akirudi anakuwa amelewa sana, tabia hizo
zilimuumiza sana Julieth kwani raha alizokuwa anazipata zote aliziona
chungu na kujikuta akiwa mtu wa mawazo na kulia siku zote, wakati
mwingine alikuwa akimpiga sana na alikuwa hataki kumsikiliza kwa chochote. Ilifikia
kipindi alimfukuza chumbani kwake akawa analala chumba cha wageni.
John hakujali kama Julieth ni mjamzito alimpiga bila ya huruma, kutokana
na matatizo kuwa mengi Julieth aliamua kumpigia simu rafiki yake wa
kike aliyejulikana kwa jina la mama Janeth ili kuomba ushauri kutokana
na matatizo aliyonayo. Akiwa
anampigia simu alikuwa chumbani bila kujua kwamba John alikuwa amejificha
pembezoni mwa mlango wa kuingia chumbani akisikiliza kila kitu
alichokuwa anamwambia rafiki yake. Akiwa anaendelea kuongea na simu John
aliingia kwa hasira sana na kumnyan’ganya simu kisha kumpiga makofi
huku akizungumza maneno makali.
“We
shetani ulikuwa unazungumza na nani?” Aliuliza John kwa hasira. “John leo
unaniita shetani? Halafu unanipiga?” Aliuliza Julieth huku machozi
yakimlengalenga. “Ndio nani
ulikuwa unamwambia mimi nakunyanyasa? We masikini nakuuliza
mwendawazimu mkubwa na nitakuua leo na simu naichukua, hutakiwi
kuwa na simu umekalia umbea tu. Nisikusikie unamwambia mtu yeyote
mimi nakutesa mwehu wewe hata ukiwaambia watanifanya nini?”
Wakati
John akiwa anasema maneno yote hayo Julieth alikuwa akilia kwa uchungu wa
maumivu. “Unanionea
John nimekukosea nini mimi.” Alilalamika Julieth huku akishikashika
na kupapasa tumbo lake. “Nyamaza
sitaki kusikia sauti yako nasikia kichefuhefu kabisa toka hapa.” Alisema
John huku Julieth akiondoka akiwa analia. Ama kweli usilolijua ni sawa na
usiku wa kiza. Julieth hakujua kwa nini John amebadilika vile ghafla na
kwamba nini kifanyike ili kumrudisha katika hali yake ya kawaida ilikuwa ni
kitu kisichowezekana ilibidi awe mvumilivu na kujipa matumaini.
Baada ya
siku kadhaa kupita hakukuwa na mabadiliko yoyote ila matatizo yalizidi
kila siku ilikuwa ni ugomvi. Miezi kadhaa ilipita bila Julieth kuwa na
mawasiliano na wazazi wake kwani alikuwa hana simu, hivyo ilikuwa vigumu
kujua hata wazazi wake walikuwa wanaendeleaje. Kwa kweli maisha
yalikuwa magumu sana. Wakati huo mimba ilikuwa na umri wamiezi saba
lakini John alikuwa hajali.
Maoni 1 :
Simulizi, kabambe, bora uwe na kitabu ili ufaidi vyema, au sio mpendwa?
Chapisha Maoni