ILIPOISHIA
Maisha yaliendelea kuwa mazuri na baba Jamal hakuwahi kugundua chochote kinachoendelea kati ya mkewe na mwanawe Jamal. Hatimaye muda wa kujifungua kwa mama mdogo uliwadia, alijifungua mtoto wa kiume na kumpa jina la Rama. Wakati huo Jamal alikuwa akimaliza Kidato cha Sita na alimpenda sana mtoto wa mama yake mdogo. Alipokuwa nyumbani alitumia muda mwingi kucheza na yule mtoto kiasi kwamba hata mama yake mdogo alifurahi sana.USIKOSE SURA YA ........15..........
INAPOENDELEA
Hatimaye
Jamal alimaliza Kidato cha Sita na matokeo yalipotoka alikuwa amefaulu
vizuri sana. Baba yake na mama mdogo wote walifurahi sana na matokeo mazuri ya kijana wao kisha walimtaka aendeleze juhudi
zaidi katika masomo ya chuo. Jamal Alijaza fomu za kujiunga na Chuo
Kikuuu cha Dar es Salaam. Aisha alikuwa amemaliza Darasa la Saba na
sasa alikuwa akisoma Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari
ya Jangwani.
Jamal
aliamua kwenda kuishi hosteli za mabibo. Lakini alikuwa akija nyumbani
mara kwa mara hasa siku za Jumamosi na Jumapili. Uhusiano wa
kimapenzi na mama yake mdogo uliendelea kila walipokutana. Jamal alishazoea
kabisa kuwa na mama yake mdogo na hata baba yake alipoona jinsi
Jamal alivyo karibu na mama yake mdogo alikuwa akifurahi sana bila kujua nini
kimewaweka karibu.
********Baada
ya miezi mitatu********
Siku moja
Jamal alipomaliza tu kufanya mtihani wa moja ya masomo anayosoma
alikwenda moja kwa moja chumbani kwake hosteli za mabibo. Baada ya
kuoga aliamua kwenda katika kiwanja cha mpira wa miguu ambako
alikaa peke yake akiwaza na kutafakari juu ya uhusiano na mama yake
mdogo.
“Nimekuwa
na uhusiano na mke wa baba yangu kwa muda mrefu sana sasa.
Kibaya zaidi nimezaa naye ingawa baba hafahamu. Kila ninapomwona
baba, nafsi yangu inanishtaki na ninaogopa sana, sina raha dunia hii kila ninapokumbuka kuhusu mama mdogo. Sijui hatima ya jambo
hili, kwani baba anajua Rama ni mdogo wangu. Lakini haya yote yasingetokea
isingekuwa ni umalaya wa mama mdogo sijui nitafanya nini.
Hili ni
kosa kubwa sana na ni dhambi mbele za Mungu. Na baba akigundua
ataniua tu! Lazima ataniua.” Aliwaza Jamal. Jamal alijiuliza maswali
mengi ambayo majibu yake hakuwa nayo. “Nadhani
nimwambie mama mdogo ili tujadili na kuamua nini cha.
Hivi hadi lini nitaendelea kukosa raha?” Aliwaza Jamal. Baada ya
kukaa takribani saa tatu pale uwanjani, Jamal aliamua kurudi chumbani
kujisomea kwani siku iliyofuata alikuwa na mtihani. Ulipofika muda wa
usiku Jamal alikwenda kulala huku akiwa na mawazo mengi sana kuhusu mama
yake mdogo na uhusiano walianao.
Kila usingizi ulipomjia alianza
kuota ndoto mbaya za kukimbizwa na mnyama wa ajabu, za kupaa hewani, kumezwa na joka kubwa, za kufeli mtihani, za kufiwa mdogo wake n.k.
Yapata saa tisa hivi za alfajiri Jamal aliota ndoto mbaya zaidi, ilikuwa ni
ndoto ya kujiwa na mama yake mzazi aliyefariki siku nyingi. Akiwa
usingizini aliota mama yake akiwa amesimama pembeni mwa kitanda chake
amevaa nguo nyeupe akimtazama huku akiwa anatoa machozi, alimuuliza
swali: “Mwanangu kwa nini umefanya hivi? Kisha alitoweka.
Jamal
alishtuka kutoka usingizini akiwa na hofu na kutweta kama mtu aliyepagawa. “Mungu
wangu nimemwona Mama! Mama nisamehe! Mama yangu nisamehe!
Uko wapi Mama?” Alipiga kelele Jamal. Baada ya
kushtuka Jamal aliamka akiwa amechanganyikiwa. Hakupata usingizi
tena hadi kulipopambazuka. Ilipofika
asubuhi Jamal alioga haraka na kuelekea nyumbani kwao kwani alijaa
hofu kubwa kuhusiana na ile ndoto. Alipofika nyumbani alimkuta mama yake
mdogo peke yake, ambaye alifurahi sana alipomwona tu Jamali.
“Jamal
mpenzi wangu nimefurahi sana umekuja nimekukosa siku nyingi sana”
Alitamka mama mdogo huku akielekea kumkumbatia Jamal. “Sikiliza
mama mdogo, huu mchezo uishe siku ya leo sasa hivi, sitaki! Nasema
sitaki! Pia hata baba sasa nitamuweka wazi yote yaliyotokea.” Aliongea
Jamal huku akimsukumia mbali mama mdogo. “He! we
Jamal una kichaa nini? Yaani unataka kumwambia nini baba yako? Sasa
naona unataka kuuwasha moto ambao kuuzima hutaweza. Ehe! na ukisha
mwambia unatarajia nini?” Aliongea mama mdogo kwa kufoka. “Natarajia
vyovyote itakavyokuwa, liwalo na liwe.” Alijibu Jamal. Mama yake
mdogo alishindwa kuelewa Jamal amepatwa na maswaibu gani akasema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni