MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
ILIPOISHIA “Mmh jamani huna hela ndogo kaka au kuna kitu kingine unataka kununua dukani nikakuchukulie, asubuhi hii chenchi zinasumbua kweli.” Alisema Julieth kwa kulalamika. “Usijali Julieth nipe hizo chapati na fedha inayobaki ni zawadi yako.” Alijibu John. “Mh we kaka, hela yote hii nibaki nayo kuna usalama kweli? Hapana kaka ngoja nikutafutie tu chenchi.” Alisema Julieth huku akinyanyuka kwenda dukani. USIKOSE SURA YA .....4.....
INAPOENDELEA
“Julieth
usiogope mimi sina nia mbaya na wewe chukua tu hiyo hela itakusaidia
usijali.” Alitamka John huku akimzuia kuondoka. Julieth
aliamua kukaa chini na kumsikiliza John hatimaye wakafahamiana. John
alikuwa ni mkazi wa Mwanza na alikuwa ni mfanyabiashara wa samaki.
Julieth alimweleza hali halisi ya maisha yao. Baada ya kufahamiana kwa siku
kadhaa walianza kuwa marafiki na baadaye John alimtaka Julieth awe mpenzi
wake. Mwanzoni Julieth alikataa sana kuhusu urafiki wa kimapenzi
na John.
Lakini baadaye alikubali wakawa marafiki. siku moja Julieth
akiwa amekaa nje ya nyumba yao John alipita pale na kufanya maongezi
na Julieth. “Julieth
tumekuwa marafiki kwa muda wa wiki tatu sasa naona nikwambie ukweli.
Kutoka siku ya kwanza nilipokuona nilitamani sana uwe mpenzi wangu.
Naomba unipe nafasi ndani ya moyo wako. Nakupenda Julieth zaidi ya
urafiki tulionao.” John alimwambia Julieth.
“Haiwezekani
John! Mimi ni masikini sana unaiona familia yetu inanitegemea
sana mimi, halafu nianze tena mapenzi! Hapana! Tena sitaki! Wewe
tafuta tu mwanamke atakayekufaa anayeendana na wewe.” Alikataa Julieth
kwa msisitizo mkubwa. “Sikiliza
nikwambie Julieth, mimi na wewe tukiwa pamoja hata familia
yako
itakuwa yangu pia, tutasaidiana sana katika maisha. Mama yako atakuwa
hana matatizo tena.
Wewe nipe nafasi amini hutajuta maishani kwa
kunikubali mimi.” John aliendelea kubembeleza. Julieth
alinyamaza kimya kwa muda huku akichimba chini na kidole gumba cha mguu
wa kushoto. “Huyu kaka
tumefahamiana kwa muda mfupi sana lakini ni mtu mwenye heshima na
amekuwa karibu na mimi kwa wakati wote. Lakini zaidi ya yote hata
mimi pia nimempenda. Nikimkubali naamni hata mama atampenda
pia. Lakini je, mama atakubali niolewe katika umri huu?”Aliwaza
Julieth huku John akimwangalia kwa macho na uso wa kumtamani.
“Nimekubali
ombi lako.” Julieth hatimaye alikubali huku akiendelea kuchimba
chini na kuangalia pembeni akijaribu kuyakwepa macho ya John. “Nimefurahi
sana Julieth nakupenda sana tutakwenda kuishi wote Mwanza.”
Aliongea John huku akimkumbatia, kumbusu na kumnyanyua Julieth
juu kama mtoto mdogo.
“Wewe!
Mimi niende Mwanza nimwache mama na nani? Hapana kwanza inabidi
nikupeleke ukamwone mama umwambie lakini hilo la kwenda Mwanza
sahau.” Julieth Alimaka na Kuhamaki.
Ilikuwa ni
siku ya furaha sana kwa wote na bila kupoteza muda wote wawili
walianza safari ya kwenda nyumbani kwa kina Julieth ili kuonana na mama.
Walipofika walimkuta mama Julieth akiwa amekaa sebuleni. Julieth
aliongoza kuingia ndani huku akifuatiwa na John. Julieth alimweleza mama yake
juu ya uhusiano wao na John.
Mama
Julieth alichukia sana kusikia eti Julieth kapata rafiki wa kumwoa. Kimsingi
mama yake hakuwa tayari kumruhusu Julieth kuolewa katika umri
mdogo. Vilevile, mama yake Julieth alikuwa bado ana ndoto ya kwamba
Julieth atasoma hadi chuo kikuu. “Julieth usijidanganye
kabisa umri wako bado ni mdogo kuhimili mikikimikiki
ya ndoa. Lakini pia mimi bado napenda ukasome ili ndoto yako ya
kuwa daktari itimie.”Alitahadharisha mama Julieth juu ya urafiki alionao na
John.
“Hapana
mama kama ni kusoma atasoma tu, na kuhusu kwamba Julieth ana umri
mdogo si tatizo kwani kuna wengine wanaolewa wakiwa na umri chini ya
umri wa Julieth, lakini wanahimili vishindo vya maisha ya ndoa.” Alifafanua
zaidi John. “Na wewe
mwenyewe muolewaji unasemaji mbona umenyamaza kimya?” Aliuliza
mama Julieth. “Mimi mama
nipo tayari kuolewa naye kwani kwa kipindi cha wiki tatu tangu
nimfahamu ameonyesha moyo wa kutusaidia.” Alijibu Julieth huku akimwangalia
John kwa macho ya kusisitiza.
“Sawa! Kwa
sababu yeye ameridhia hata nikimkatalia ni kazi bure. Ila nawaomba
mfuate taratibu zote za kimila na kufunga ndoa rasmi ili mpate baraka
kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa wazazi pia.” Alishauri mama Julieth. USIKOSE SURA YA ......5........
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni