Habari yako Adela mimi ni mwanamume nina mke na watoto watatu tumeishi kwenye ndoa takribani miaka kumi sasa kuna kipindi mke wangu alinifumania nikiwa na mwanamke mwingine ni siku ambayo siwezi kuisahau kwani nilikuwa sina cha kujitetea ilinibidi nikubali nakuomba msamaha kwa kilichotokea huku nikiwa na nia ya kubadilika na kutorudia kosa.
Mke wangu alinisamehe lakini sikujua kumbe alikuwa na kinyongo moyoni mwake hivi majuzi nilimfumania kwenye ujumbe mfupi akiwa anawasiliana na mwanaume mwingine ikionyesha kabisa wana mahusiano ya kimapenzi ukweli ni kwamba iiliniuma sana bado kidogo nimpige nilimuuliza kwa vitisho akaniambia ameamua kufanya hivyo kwasababu na mimi nilimsaliti kitendo hiki kimeniumiza hadi natamani kumfukuza nyumbani kwangu amenikera sana sina amani.
Maoni 5 :
Kwani yeye alipokufumania alikufukuza nyumbani? si alikusamehe? Kwa nini wewe unaona hasira badala ya kumsamehe na kujua sasa ngoma droo hakuna atakayerudia tena maana wote mmelipizana kisasi.Msamehe na wewe acha udume huo wakati wewe ndiye mwanzilishi wa sokomoko hilo.Huna hata haya kuja kulalamika hapa wakati ukweli unaujua.Msameheeeeee kama alivyokusamehe wewe yaishe basi!!
Kumbe kwako inauma ila kwake haikuuma eti? Wanaume mna mambo kaaa! Swamehe kama ulivyosamehewa!
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. itabidi amsamehe tu.
Haswaaaaaaa? Mkuki kwa nguruwe!!! Pambafu msamehe mwenzio acha kuwa kidume wa mabavu
Mmmh! we mwanaume unachekesha sana kwani yeye alivyokusamehe alikuwa mjinga? wewe ulilianzisha na yeye kalimaliza, hiyo ni ngoma droo.
samehe saba mara sabini nawe utasamehewa. kilichokufanya utoke nje ya ndoa yako ni nini???
Chapisha Maoni