Jumatano, Novemba 07, 2012

SIMULIZI YA MAMA MDOGO SURA YA .....13.....



KITABU  MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI  ADELA DALLY KAVISHE

ILIPOISHIA Baada ya maongezi hayo Goodluck aliaga na kuondoka kuelekea kwao akimwacha Jamal akiwa na mawazo mengi kuhusu mama yake mdogo. Siku iliyofuata yapata saa nne asubuhi wakati babake akiwa kazini Jamal alimfuata mama yake mdogo sebuleni ili azungumze naye kuhusu swala la kupekekwa shule. Alipoingia tu alimkuta amekaa katika sofa akifuma kitambaa.


INAPOENDELEA: 
“Habari za asubuhi mama mdogo? Alisalimia Jamal. “Nzuri Jamal umeamkeje? Ah! Salama kabisa” Alijibu Jamal. “Vipi Jamal mbona unaonekana mnyonge sana, unaumwa?”Aliuliza mama mdogo. “Hapana mama mdogo, nina shida na wewe.” Alisema Jamal. “Heeh! Makubwa na wewe huwa unashida? Haya hebu sema unashida gani?” Alishangaa na kuuliza mama mdogo kwa kebehi. Unajua mama mdogo mimi napenda sana kusoma, baba anaonyesha hataki tena kunisomesha. Lakini ninauhakika nikikutumia wewe anaweza kubadili msimamo wake. Tafadhali naomba unibembelezee.” Alitamka Jamal. “Jamal tatizo siyo baba yako hataki kukupeleka shule. Ila tatizo ni wewe mwenyewe hutaki kwenda shule.” Alisema mama mdogo huku akiweka kitambaa juu ya meza na kusogea kwa Jamal.

“Hapana mama mdogo mimi shule napenda sana.” Alijibu Jamal. “Hapana kama unapenda shule usingekuwa unanikatalia ombi langu siku zote hizi.” Aliongea mama mdogo huku akirembua macho. “Jamal mimi nakupenda sana na unajua fika kwa nini unakataa ombi langu? Hivi huoni kama unateseka bure kwa ujinga wako?” Aliuliza mama mdogo. Jamal alinyamaza kimya kidogo huku wakiangaliana na mama mdogo.
Mama mdogo alitabasamu kimahaba kisha akaangalia chini kwa aibu. “Unajua mama mdogo hilo ni jambo la hatari sana, baba akigundua ataniua.” Alitahadharisha Jamal.

“Usiwe mwoga kiasi hicho Jamal, hawezi kugundua kabisa kwani tutafanya siri. Isitoshe baba yako huwa anasafiri mara kwa mara, je, atajuaje?” Alisema mama mdogo. Jamal aliinamisha kichwa chini akawaza kitu, kisha akashusha pumzi kwa nguvu huku akimwangalia mama mdogo kwa tabasamu na uso wa kukubali. “Sawa mama mdogo mimi nimekubali, ila nataka umwambie baba suala la mimi kwenda shule, nikasome shule yoyote ile, kwani wenzangu niliomaliza nao tayari wameshaanza masomo inaniuma sana.” Alisema Jamal.

Baada ya Jamal kukubali ombi, mama mdogo alisimama na kumkumbatia Jamal huku akimbusu mara kadhaa kwenye mashavu. Mama mdogo alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kimapenzi. Alishindwa kuamini kama Jamal amekubali. “Hakuna tatizo Jamal kila kitu kitakwenda sawa, yaani utasoma unavyotaka na kila kitu utapata niamini nakupenda sana.” Aliongea mama mdogo huku akimpapasa Jamal sehemu mbalimbali na kumbusu. “Yote haya nayafanya kwa sababu sina namna nitafanya nini lakini ipo siku na mwachia Mungu.” Aliwaza Jamal huku naye akimkumbatia mama yake mdogo. Jamal na mama mdogo wamefungua ukurasa mpya wa maisha. Uhusiano
wa mtoto na mama mdogo umekufa, bali sasa ni wapenzi. Baba Jamal aliporudi kutoka kazini mke wake alimwambia kuhusu kumpeleka Jamal shule. 

Ilikuwa ni jioni tulivu Jamal, mama mdogo na baba yake Jamal walikuwa wapo mezani wakila chakula. “Baba Jamal mimi naona bora Jamal angekwenda Kidato cha Tano kwani ni muda sasa amekaa nyumbani. Kumbuka elimu pekee ndio urithi kwa mtoto.” Aliongea mama mdogo huku akimwangalia baba Jamal. “Je, kama alitaka kusoma angejihusisha na mapenzi kwa umri huu? Ameniudhi sana muache akae kwanza nyumbani.” Alitamka baba Jamal. “Akikaa nyumbani hatutakuwa tumemsaidia, basi aende hata shule ya kutwa ili jioni awe anarudi nyumbani.” Alibembeleza mama mdogo.
“Ahm! Tutaongea baadaye naona mnazidi kunichanganya.” Alitamka baba Jamal huku akimkonyeza mama mdogo.

Usiku mama mdogo alianzisha tena mazungumzo na baba Jamal kuhusu kumpeleka Jamal shule. Alimsifia Jamal kwamba amebadilika sana na kwamba sasa ni mtoto mzuri, hana kiburi, anajituma katika kazi na ameacha kabisa mambo ya mapenzi. Hivyo alisisitiza kwamba apelekwe shule ili akasome kwa faida yake na mdogo wake. Baada ya kufikiria sana baba Jamal alikubali na kumtaka mama yake mdogo aende shule ya Sekondari ya Jitegemee ili akatafute nafasi na kisha Jamal aanze kusoma mara moja. NINI KITAENDELA USIKOSE SURA YA 14 ,,,,,,,,,,,,,,,,

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom