Jumatano, Aprili 11, 2012

Nimegundua ni mume wa mtu nataka tuachane yeye anasema atanichinja akinikuta na mwanamume mwingine

Habari yako Adela mimi ni moja kati ya wadau wazuri sana wa blog yako nina shida nilikuwa na mwanamume ambaye mwanzoni wakati tunaanza mahusiano aliniambia hana mke, lakini cha ajabu nimekaa naye takribani mwaka mmoja alinifuata dada mmoja nakuniambia niachane na mume wake nilipofanya uchunguzi kweli nimegundua ni mume wa mtu baada ya kufahamu maamuzi yangu ni kuachana na huyu kaka kwani alinidanganya na mimi nilikuwa nampenda sana niliamua kuacha kupokea simu zake.

 Alinifuata na kuniambia haitatokea mimi na yeye tuachane na akinikuta na mwanamume mwingine ananichinja kuna siku alinikuta nimekaa bar na marafiki zangu alianza kunipiga na kunirudisha nyumbani inaniuma anavyoyafuatilia maisha yangu huku akinipa vitisho sijui nifanyeje naombeni ushauri mimi simtaki

Maoni 7 :

Tausi Usi Ame Makame alisema ...

Mume wa mtu halafu anataka kukuchinja akigundua unatembea na mtu? Huyo mume anapaswa akatwe mb... na mkewe kwanza kabla hajafikiria kukuua wewe....

Mwache huyo asikupotezee muda.

Tausi Usi Ame Makame,
Oslo,
Norway

Bila jina alisema ...

yaani watu wengine bwana..wanajifikiriaga wao tu! nakushauri dada ukamripoti huyo kaka polisi ili akuache uendelee na maisha yako kwakuwa na ushahid upo kuwa ni mume wa mtu. isije ikatokea kweli akakufanyia kitu kibaya na ukose pa kukimbilia ila ukiwaambia polisi na ndugu zako wako wa karibu utakuwa kwenye safe side.

Bila jina alisema ...

Yaani huyo mwanamume ni mwehu achana naye kabisa

Bila jina alisema ...

heeeee kama ni mimi namshataki kabisa huyo gumegume

Bila jina alisema ...

Achana naye kabisaaaaaa.Yaani amefikia hatua ya kukupa kipigo kwenye bar mbele ya watu?yaani yeye hajitambui kuwa ni mume wa mtu.Wewe kimbia sana na mwambie kama ni kuua niue lakini sihitaji kuwa na wewe kwa sababu ni mume wa mtu. Inaelekea ulikuwa unampa vitu vitamu sana wewe dada.Pole na mkasa huo,lakini hakuna njia wewe kimbia usipoacha hapo ndipo utapata kipigo kikubwa kwani yule mke wake anaweza kukualikia vijana wa msituni wakakufanyizia.

Bila jina alisema ...

Mshukuru mungu wako kwani kakuonyesha huyo mwanaume ni tapeli tu kama kakudanganya kuwa hana mke na ukamwamini atashindwaje kukuambukiza ukimwi kama anao?? Watch out!

Bila jina alisema ...

dada mume wa mtu ni kama nukisi kwenye maisha ya bint ambaye ajaolewa . atakuja kukufanya ukose ata mchumba. mshitaki polisi na pia polisi wa mwite yeye na ikiwezekana na mkewe wamwambie live na kama una mchumba awepo na uyo gumegume atambulishwe kuwa wewe ni mchumba wa mtu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom