Pages

Alhamisi, Machi 14, 2013

"Anadai mtoto wakati hakutoa matunzo"

Kuna baadhi ya wanaume wanatabia ya kukimbia malezi ya mtoto na hivyo kumuachia mama jukumu la kumlea mtoto peke yake huku yeye akiendelea na starehe za maisha yake lakini baadaye mtoto akikua huanza kuonyesha dalili za kumtaka mtoto. Kuna dada mmoja anaitwa Sara yamemtokea anaomba ushauri. 

 "Nilipata mimba nikiwa bado nasoma chuo,  kipindi hicho bwana aliyenipa mimba aliikataa nikalea mwenyewe tena kwenye mazingira magumu sana huku nikisemwa sana na ndugu zangu, baadaye nilimpata mchumba mwingine ambaye alikubali kuishi na mimi pamoja na mtoto wangu, na hadi hivi leo naishi naye na mtoto wangu anapata malezi mazuri, na shule anamlipia ada vizuri, anasoma darasa la kwanza sasa cha ajabu yule bwana ambaye ni baba wa mtoto wangu  anataka mtoto huku akidai kwamba atanishtaki nisipompa mtoto wake na wakati mwingine anamfuata huyu mume wangu nakumuambia mimi ni mke wake yaani ananisumbua sana na mimi sitaki amchukue mtoto wangu sijui nifanyeje naombeni ushauri.

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

Alipokataa kuwa siyo mimba yake ulihitaji kuandikishana naye ili baadaye asije kumdai.Inaelekea alikataa kwa sababu alijua atahitajika mahitaji ya mtoto.Lakini ukweli upo palepale kwamba ni mtoto wake ila njia anayotumia kumtaka mtoto siyo sahihi.Sidhani hata kama atakushitaki ina maana yoyote maadamu hajawahi kumlea kuna taratibu nzuri tu za kufuata.Atahitaji kukulipa matumizi yote ya mtoto.Watu wa ustawi wa jamii watakusaidia nenda huko waeleze kunachojiri.

Bila jina alisema ...

Nakushauri nenda ofisi za ustawi wa Jamii, au TAWLA au TGNP ukawaele tatizo lako na kuomba ushauri wa kisheria watakusaidia na kumtia adabu huyo kijana anayetaka kukuharibia nyumba yako.

Bila jina alisema ...

Tafuta mwanasheria uongee nae, utajua nini cha kufanya. Mwanaume huyo hafai kuwa baba kwa sababu alishakimbia majukumu toka mwanzo.Pole sana dada Mungu ni mwena sana ukimtumainia yeye utapata ufumbuzi.

Bila jina alisema ...

KIRUUU MWAMBIE MIMBA HAIKUW YAKE ULIKUW UNAMBAMBIKIZIA AILI AACHE KUKUSUMBUA NAJUA HATOKUW NA UWEZO WA DNA LOL..KM ULIMUANDIKISHA UBINI WA HUYO JITU JINGA IMEKULA KWAKO...MIE NIN NDUGU YANGU ALIPATA SHESHE KM HII BAHATI MTOTO ALIMUANDIKISHA UBIN WA WA UKOO WAO.. ALIVYOJILETA AKAMWAMBIA HAIKUWA MIBMBA YAKE MPAKA LEO ANAJIFANYA KUOMBA MSAMAH..

Bila jina alisema ...

yaani kama yalionikuta, kwanza mpeleke polisi kwamba anakufanya fujo wewe na familia yako, hatakama kidamu ni baba yake lakini alimtupa na mwingine ndio amwemwokota hata aende wapi hataweza kumchukua mtoto. so asikusumbue hata kidogo! all the best!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom