Pages

Jumapili, Machi 17, 2013

ANAOMBA USHAURI "nimeolewa tatizo ni kwamba simpendi mume wangu"

habari dada Adela,   naomba unisaidie kuniwekewa ujumbe wangu kwa wadau wapate kunisaidia, email yangu kapuni tafadhali,    Mimi ni msichana miaka 21, nimeolewa, tatizo ni kwamba simpendi mume wangu hata kidogo, miezi mitatu ya mwanzo nilimpenda ila alivyoniambia tu kuwa ana mtoto sikuwa tena na mapenzi naye kwani sikuwa napenda kuwa na
mwanaume mwenye mtoto maana hawa mara nyingi wanaletaga matata wanajifanya kutokuwa tena na mapenzi na wanawake waliozaa nao kabla ya ndoa lakini wanawarudia, sasa nimevumilia mpaka nimechoka najilazimisha lakin yaani moyo wangu umekataa kabisa na nimezaa naye mtoto mmoja, natamani kuachana nae lakini wazazi hawakubaliani na hili, naombeni
ushauri nifanyeje? Asanteni

Maoni 9 :

emu-three alisema ...


Ni kweli watu wanaweza wakakutana na hata kufikia hatua ya kuoana, na baadaye wakagundua kuwa hawapendani, kwasababu kadhaa.

Swali la kujiuliza ni kwanini mlipendana awali na sasa pendo hilo limechuja?

JE sababu hizo zinatokana na utashi wako mwenyewe au, ni kutokana na ushauri wa watu wengine?

Je mumewahi kukaa na kuelezana hayo kabla ya ndoa kuwa mimi sitaki hiki na kile na mkakubaliano hayo, na baadaye yakatokea kinyume na makubaliano yenu?

Je hakuna mengine mengi unayapenda kutoka kwake? Je wewe mwenyewe umkweli kiasi gani...nk.

Huenda mlitamaniana tu, kwa sababu ya mvuto wa kimaumbila, kwasababu ya pesa, au sababu yoyote ile, na sasa ile sababu haipo tena.

Kwa tatizo lako, umesema mumeo `amekudanganya' swali je wewe tangu uolewe na huyo mumeo hujawahi kufanya jambo la `kumdanganya' mumeo,....kibinadamu kila mmoja anakosea.

Cha muhimu, kwa vile mumeshaoana, na hata kufikia hatua ya kupata mtoto, ni vyema, mkapeana muda, katika muda huo, mkaambiana ukweli,...kuwa kila mmoja afunguke aeleze ukweli kuhusu yeye mwenyewe, kama ana mtoto, ana jambo fulani,....ili uelewe na yeye aelewe yako uliyo nayo, hapo mnajenga `uaminifu'

Tusitafute kisingizio fulani kwa ajili ya `kuachana' maana huna uhakika kuwa huyo utakayekuja kukutana naye tena, atakuwa `msafi kihivyo'.

Kwa binadamu tulivyo hasa karine hizi,huwezi ukampata aliye msafii kamili, ni bahati sana, wengi wetu tumejikuta na mitihani hii na ile, lakini mtu huyo huyo anaweza akawa na mengi mema, kwani huyu anaweza akawa na hili na asiwe na lile, kama ulivyo wewe, lazima una ambayo mwenzako hayapendi lakini anavumilia...sote sio wakamilifu.

Nikuambie ukweli, huyo huyo, mnaweza mkalienzi pendo lenu mkawa mnapendana kama vile mpo kwenye fungate,...kaeni , elezaneni, na tubuni yale mliyofanya kabla ya ndoa yenu. Msisikileze majirani na wale wanaojifanya ni marafiki, hawo ni maadui wa siri....

Mimi nina uhakika, kama kweli mlipendana awali, mtapendana tena, `mkitaka iwe hivyo' kwani mvunja ndoa na mvunja pendo, ni wanandoa wenyewe, na mjengaji wa ndoa, na muenziji wa pendo ni wanandoa hawo hawo wengine ni wapiga debe tu.

Bila jina alisema ...

asante emu, ukweli ni kwamba hapo mwanzo tunakutana hata hakuwa na pesa kwahiyo sikuwa nampendea pesa wala sikutaman chochote kutoka kwake zaid nilikua nampenda kwel ila alivyoniambia tu anamtoto mapendo yakakata hapohapo, ni kweli wote hatujakamilika lakn nitavumilia mpaka lini nitaishi maisha yakuvumilia mpaka lini. Nashkr kwa msaada Nitazid kujitahidi labda mambo yatabadilika

Bila jina alisema ...

Ni vigumu sana Kuishi na mtu usiyempenda haijalishi Ana pesa kiasi gani wewe jipange bora muachane lakini kuwa makini usije kujuta baadaye

Bila jina alisema ...

Makubwa haya usimuache mume wako Shost Kama Angekuwa anampenda huyo aliyezaa Naye Si angemuoa acha utoto mume mtamu utajuta

Bila jina alisema ...

Ukimuacha mume ako utajuta vumilia shoga yangu unaweza kusema cha nini kwasababu unacho kumbe mwenzio anakupenda kutoka moyoni

Bila jina alisema ...

Kwani ulichokipenda huko mwanzo kimeenda wapi tena?Huo ni utoto.Ungetuambia kuwa mumeo hakupendi sawa labda tungeelewa.Kama wewe ndiye humpendi na uliolewa naye hilo gubu linatoka wapi?Au ulimwendea kwa waganga wa kienyeji na dawa zimechuja hazipo tena kupenda?Sababu unayotoa kutompenda tena ni dhaifu mnoooooo.Zinduka utapata kichaa bure!!

Bila jina alisema ...

asanteni wapendwa kwa ushaur kilamtu kwa namna yake alivyonishaur mana yani nakatatamaa ya maisha sina raha nitajitahid,mwenye mada

Bila jina alisema ...

USHAURI WANGU .FANYA IBADA MRUDIE MUNGU TUU KWANI DUNIA NI KIGEUGEU .KUMBUKA UNAWEZA KUOLEWA NA MUME AKUPENDAYENA ASIYE NA MTOTO NA MKAKAA NAE MAISHA MAZURI NA MEMA .BAADA YA MIAKA UNA WATOTO, AKAZAA NJE JE UTAACHIKA KUNA MASWALI MENGI JIULIZE NA USIMCHUKIE HUYO MTT WA NJE HANA KOSA .KWANI UMEMCHUKIA MWAUME KISA MTOTO
KUMBUKA HAKUNA MWAUME BIKIRA

Bila jina alisema ...

si mbaya kama ni mwisilamu omba talaka na kama ni mkristo fata sheria za kuvunja ndoa. ila fikiri kabla ya kutenda usije ukaruka majivu ukakanyaga moto

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom