Jumatatu, Januari 30, 2012

"Simpendi mwanamume anayetaka kunioa nahisi nitaolewa kwa kuogopa laana ya wazazi"

Mimi ni mwanamke naishi na wazazi wangu ambao nawapenda sana wamenilea na kunipa kila ninachokitaka nimesoma na kwa sasa nafanya kazi tatizo linakuja hivi karibuni wazazi wangu walinitambulisha kwa mwanamume ambaye wanataka mimi niolewe naye ukweli ni kwamba mimi huyo mwanamume sijampenda na pia anaumri mkubwa kuliko hata mimi yaani anaweza hata kuwa baba yangu,, ila baba na mama wananiambia nisingesoma hadi hapa nilipo bila ya huyu mwanamume kwani amekuwa akiwasaidia wazazi wangu kwa kiasi kikubwa na alinipenda mimi tokea nikiwa mtoto mdogo,, binafsi mimi ninaye mchumba ambaye nimemueleza hali halisi alichoniambia mchumba wangu nitoroke nyumbani nikaishi mbali yeye atanisaidia,, lakini nikifikiria mimi ni mtoto wa pekee kwa wazazi wangu nilikuwa na kaka na mdogo walishafariki zamani kidogo,,  na pia wazazi wangu wananiambia nisipoolewa na huyo mwanamume waliyenichagulia  wataniachia laana hapa nilipo nakosa raha kila nikifikiria kuanza maisha na mtu nisiyempenda naombeni ushauri wenu

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

Kwanza akae akijuwa kwamba hakuna laana inayotoka kwa wazazi ambayo Mungu ataikubali kama ya kuhusu ndoa, laana kama hiyo Mungu haikubali kabisa, na kama inavyojulikana ndoa Inapangwa Mbinguni, so kama Mungu kapanga ataolewa na kama hajapanga basi haolewi, ila pia siokila jambo umsubiri Mungu, kama nayeye hataki kuolewa basi asiulazimishe moyo wake kwa furaha ya wazazi na machungu kwake, Aonyeshe Juhudi binafi za kuchukia ndoa kama hiyo kwa vitendo na Mungu atamsaidia.

Bila jina alisema ...

Fikiri mara2 mingne ni mitihan ya Mungu.. Unaweza kukataa ikaja kukubadilishia story hapo badae

Mimi alisema ...

Do what ur heart tells you to do.. forget about those stupid comment of ur parent.. Ukiolewa wewe ndio utaishi na huyo baba na sio wazazi wako..

Mie kuna shoga yangu alitafutiwa na mama yake mchumba kisa ana hela ni tajiri shoga akakataa, mama akaitisha kikao cha ndugu kumsemea shoga yangu, ila bidada mbele ya ukoo akasema kama mama anaona huyo bwana ni tajiri kwa nini asiolewe yeye (mama mwenyewe coz hana mume) watu mdomo wazi akainuka na kuondoka.. Mpaka leo hajaolewa ila ni bora kuliko kuolewa na mwanaume usiyempenda...

Bila jina alisema ...

Acha nidhamu ya uoga bwana unaogopa lawama ya wazazi mana yake nini hivi wewe the way unaonekana unaogopa wazazi kuliko hata aliyekuumba nakuonea huruma.

JOEMA alisema ...

POLE DADA FATA MOYO WAKO USILAZIMISHE NDOA KWANI NDOA NI AGANO LA MILELE UKIOLEWA NA MTU USIYEMPENDA UTAJUTA MAISHA YAKO YOTE ENDAPO ATAKUNYANYASA AU MKIGOMBANA KIDOGO TU TATIZO LITAKUWA KUBWA TOFAUTI UKIOLEWA NA MTU UMPENDAE ATA KUKIWA NA TATIZO NI RAISI KUVUMILIA NA KUSEMA AAAH NDIO HALI YA NDOA UTACHUKULIA KWA URAHISI SO THINK TWICE BEFORE UJAFUNGA HIYO NDOA ,NDOA SI MAJARIBIO

Bila jina alisema ...

dada usikubali kuolewa na mtu usiempenda chakufanya mwite,uyo baba mkae mahali ukiwa na mtu mwingine mzima ata ukiweza mtafute mchungaji au mzee wa usharika au mkuu wa ukoo wenu na umweleze wazi kuwa hauko tayari kuolewa nae. wasipokusikiliza kimbia utorokee mbali.best wishes

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom