Utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya katika sehemu mbalimbali unaonyesha kuwa pombe ina athari kubwa na mbaya hasa kwa kina mama wajawazito na matatizo wanayoyapata yanafahamika kitaalamu Fetal Alcoholic Syndrome (FAS). Watoto wengi wanaozaliwa na tatizo hili wanakuwa na nyuso ambazo siyo za kawaida, (fasial deformities). Watoto hawa wanaweza kuwa na pua bapa na macho yaliyoingia ndani au kupata matatizo ya kusikia na kutokuwa na uwezo wa kusoma.
Na wataalamu wanasema ni vigumu kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili na mara nyingi ni kwa watoto kabla ya kutimiza miaka kati ya mitatu na minne. Dalili zinazoonyesha mtoto ana tatizo hili ni kwanza haonyeshi dalili ya kulia au anaweza kulia kwa kiasi kidogo, huchelewa kutembea na hata kuongea, haonyeshi kuvutiwa na mazingira yanayomzunguka yaani hata kama kuna vitu vya kucheza hapendi kujishughulisha navyo.Ukiona dalili hizi nenda kituo cha afya.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni