UKOSEFU WA CHOO Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho
aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni
na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha,
kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini,
hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.
2.UGONJWA WA MOYO Kiwango
kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’
vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na
magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!
3. SHINIKIZO LA DAMU Virutubisho
vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa,
husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood
pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.
4. UGONJWA WA MAPAFU Chungwa
pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron),
virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu,
ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa
muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
5. MIFUPA NA MENO Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.
6. AFYA YA NGOZI ‘Anti
oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili
isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza
kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.
7. KOLESTRO Virutubisho
vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango
cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la
lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.
8. UKUAJI WA UBONGO Chungwa
moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini
kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo
kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.
9. KINGA YA MWILI Vitamin
C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni
muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara,
huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.
10. UGONJWA WA FIGO Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.
11. VIDONDA VYA TUMBO Unapokuwa
na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga
dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa
machungwa utakupa ahueni.
12. UGONJWA WA MAFUA Kutokana na
wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara
kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama
vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula
machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
13. KINGA YA MAGONJWA MENGI Chungwa,
siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia
hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi
(arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na
kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili
kupata faida h |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni