Ijumaa, Januari 31, 2014

CHONDE CHONDE ULEVI WAONGEZA SARATANI YA NGOZI KWA ASILIMIA 50

Unywaji wa pombe kwa wingi unadaiwa kusababisha saratani ya ngozi aina ya milanoma, Watu wanaokunywa  chupa moja ya pombe kwa siku wana hatari kwa asilimia 10 ya kupata aina hiyo ya saratani ukilinganisha na wale wanaokunywa mara mojamoja

Wanaokunywa chupa mbili kila siku wana hatari kwa asilimia 18 ya kupata saratani hiyo ya ngozi ambayo inawaathiri zaidi vijana.Wanywaji sugu ambao hunywa glasi  nne kila siku, wapo katika  hatari kwa asilimia 55 kutokana na taarifa za kimataifa za watafiti. Chupa moja ya pombe ina gramu 12.5 ya kilevi ambayo inatajwa kusababisha mabadiliko ya kibiolojia na kuifanya ngozi  kuathirika kwa urahisi na jua.

Haijafahamika moja kwa moja ni kwa namna gani pombe inachochea saratani lakini watafiti hao wanaamini kuwa ethanol ikibadilika na kuwa kemikali huweza kuchangia kuongezeka kwa saratani hiyo.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom