Jumatano, Mei 15, 2013

USHAURI WA ANGELINA JOLIE, KWA WANAWAKE BAADA YA KUKATWA MATITI KUZUIA SARATANI.

Mchezaji filamu mashuhuri kutoka Marekani. Anjeline Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.Ni kutokana na kufanyiwa  uchunguzi wa chembechembe  zake na kugunduliwa kwamba alikuwa na hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti.Anjelina mwenye umri wa miaka 37 na mama wa watoto sita alimpoteza mama yake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti. Kulingana na Jolie madaktari walisema  uwezekano wake kupata saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 za uwezo wa kuugua  saratani ya mfuko wa uzazi

Amesema "Niliamua kuchukua hatua mwenyewe  ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua saratani hiyo alisema Jolie".Kwa mujibu wa BBC , Jolie alisema  kuwa shughuli hiyo ilianza februari na kukamilika april mwishoni.Bi Jolie alieleza kuwa Mama yake alipambana na ugonjwa wa saratani kwa miaka 10 na kufariki akiwa na umri wa miaka 56.Amesema alielewa fika siku moja atawahi kuugua saratani na ndiyo maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti .
Alimsifu mumewe Brad Pitt kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila hatua aliyopitia na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanaye hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji.

Amesema "Ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi nilioufanya nakwakua ninabakia kuwa manamke hata baada ya kuondoa viungo hivyo" na kwa mwanamke yeyote  anyesoma maneno haya natumaini kuwa  anaweza kujua anaweza kuchukua maamuzi kama yangu iwapo atajigundua anazo dalili za ugonjwa wa saratani.Mwigizaji huyu  ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.

Maoni 2 :

Sebastian alisema ...

dah inapaswa wanawake wa tz kuiga jambo alilofanya jolie kwa ajiri ya kuokoa maisha yake saratani ni mbaya sana,..

Sebastian alisema ...

WANAWAKE WA KITANZANIA HAWANA BUDI KUIGA MFANO

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom