Jumatano, Mei 15, 2013

HAPPY FAMILY DAY

Kila mwaka maadhimisho ya siku ya familia duniani yamekuwa yanabeba kauli mbiu mahususi "IMARISHA NA ENDELEZA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO WA FAMILIA NA MAKUNDI MBALIMBALI YA JAMII". Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha, kuhimiza,kuelimisha familia na jamii kuendeleza mahusiano kati ya vizazi na vizazi, Familia na rika mbalimbali ili kuleta mshikamano ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.

Lengo kuu la kujenga ushirikiano katika jamii ni kuyaleta  pamoja makundi yote katika jamii na hasa makundi ya watu wanyonge, katika mustakabali wa mchakato ya maendeleo ya familia na taifa lao
Ushirikiano na mshikamano ni nguzo ya malezi bora katika familia.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom