Jumatano, Juni 20, 2012

NYOTA WA LEO CHRIS BROWN

Christopher Maurice "Chris" Brown (amezaliwa tar. 5 Mei, 1989) ni msanii wa muziki na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Ameanza kutoa rekodi yake ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2005 yenye jina sawa na lake, yaani, Chris Brown akiwa na umri wa miaka 16. Albamu ina kibao kikali cha "Run It!", ambacho kilifikia nafasi ya juu kwenye Billboard Hot .


Licha ya kupata mafanikio makubwa akiwa kama msanii wa kujitegemea, Brown amepata kushirikishwa kwenye vibao vingine vikali kama vile "No Air", aliimba pamoja na Jordin Sparks, "Shortie like Mine" sambamba kabisa na rapa Bow Wow na "Shawty Get Loose" na Lil Mama na T-Pain. Kibao hicho kilishika nafasi ya tatu, namba tisa na kumi kwenye chati za Billboard Hot 100 mfululizo


Kutokana na utaratibu wake wa kucheza, Brown amefananishwa na wasanii kama vile Usher na Michael Jackson,

Mnamo 2009, Brown alishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mwandani wake - mwimbaji Rihanna, na akapigwa kifungo cha nje cha miaka mitano na miezi sita
Tetesi za hivi karibuni ni kwamba Rihanna na Chris Brown waamerudiana na hata kupelekea ugomvi baina ya Drake na Chris Brown uliosababishwa na wivu wa kimapenzi hadi kutupiana vyupa.

Maoni 1 :

emuthree alisema ...

Tupo pamoja!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom