Kwanini mzee huyu ni maarufu?
Kwa hakika sifahamu yote juu ya mzee huyu anayependwa mno si tu kwake huko Afrika Kusini bali pia duniani kote kwa ujumla, hilo ladhihirika kwa Umoja wa Mataifa (UM) kumtengea siku maalum ya kumuenzi.
Mandela, alifungwa katika magereza tofauti kwa jumla ya miaka 27; umri wa kijana aliyekomaa. Mwanasiasa huyo, ambaye alikuwa pia Mwanasheria, mwanamichezo na mpigania haki za watu, alifungwa na serikali ya Makaburu kwa walichokiita uhaini. Nelson Mandela moja ya vijana walionzisha madai ya uhuru kwa njia ya mapigano alikuwa na imani kuu juu ya haki sawa kwa watu wote. Aliamini na anaamini kuwa binadamu wote ni sawa katika misingi ya ubinadamu- kwa haki na mahitaji yetu. Ni kwa imani na msukumo huo wa kudai uhuru na haki za watu wote wa Afrika Kusini ndo alikuwa tayari kudai haki hizo hata kama ingemlazimu kuyatoa maisha yake; funzo kubwa hilo. |
Maoni 1 :
Huyu ni mkongwe wa viongozi wenye hekima ,busara na ushupavu aliyebakia!
Chapisha Maoni